Waebrania 3:14-16
Waebrania 3:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni. Maandiko yasema hivi: “Kama mkisikia sauti yake leo, msiwe wakaidi kama wakati ule waliponiasi.” Ni akina nani waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri.
Waebrania 3:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; kama inenwavyo, Leo, kama mkisikia sauti yake, Msifanye mioyo yenu kuwa migumu, Kama wakati wa kuasi. Maana ni akina nani walioasi, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
Waebrania 3:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
Waebrania 3:14-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho. Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.” Basi ni nani waliosikia lakini bado wakaasi? Je, si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose?