Ezra 5:3-4
Ezra 5:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye Tatenai, mtawala wa mkoa wa magharibi ya Eufrate, Shethar-bozenai na wenzao, walikwenda Yerusalemu na kuuliza, “Nani aliyewaamuru kuijenga nyumba hii mpaka kuimaliza?” Pia waliuliza, “Ni akina nani wanaojenga nyumba hii? Tunataka majina yao.”
Ezra 5:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakati ule ule Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni gani?
Ezra 5:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati ule ule Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani na nani?
Ezra 5:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati ule Tatenai mtawala wa ngʼambo ya mto Frati na Shethar-Bozenai na wenzao waliwaendea, wakawauliza, “Ni nani aliyewapa ruhusa ya kujenga tena Hekalu hili na kurudishia upya kama lilivyokuwa?” Pia waliwauliza, “Je, majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani?”