Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra 5

5
Ujenzi wa hekalu waanza tena
1 # Hag 1:1; Zek 1:1 Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli. 2#Hag 1:12-15; Ezr 6:14; Mhu 12:11; Hag 2:4-9 Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia. 3#Ezr 6:6 Wakati ule ule Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? 4Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni gani? 5#2 Nya 16:9; Ezr 7:6,28; Zab 33:18; Isa 41:10; 1 Pet 3:12 Lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie hadi habari ile imfikie Dario, ndipo jawabu itakapopatikana kwa waraka.
6 # Ezr 4:9 Hii ndiyo nakala ya waraka ambao; Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto; walimtumia mfalme Dario. 7Walimtumia ripoti; na maneno haya yakaandikwa ndani yake;
Kwa Dario, mfalme Salamu sana. 8Na ajue mfalme ya kuwa sisi tuliingia nchi ya Yuda, tukafika kunako nyumba ya Mungu mkuu, iliyojengwa kwa mawe makubwa, na miti imetiwa katika kuta zake, na kazi hii inaendelea kwa bidii, na kusitawi katika mikono yao. 9Ndipo tukawauliza wale wazee, tukawaambia hivi, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? 10Tukawauliza pia majina yao, ili kukuhakikishia, tupate kuandika majina ya watu waliokuwa wakubwa wao. 11#Yos 24:15; Zab 119:46; Yon 1:9; Mt 10:32; Lk 12:8; Mdo 27:23; 1 Fal 6:1 Wakatujibu hivi, wakasema, Sisi tu watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi, nasi tunaijenga nyumba iliyojengwa zamani sana, yapata miaka mingi, ambayo mfalme mkuu wa Israeli aliijenga na kuimaliza. 12#2 Nya 34:24,25; 36:16,17; 2 Fal 24:2; Yer 39:1 Lakini hapo baba zetu walipomkasirisha Mungu wa mbingu na nchi, hata akaghadhibika, akawatia katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Mkaldayo, naye ndiye aliyeiharibu nyumba hii, akawachukua watu mateka mpaka Babeli. 13#Ezr 1:1 Lakini katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Babeli, Koreshi, mfalme, alitoa amri ijengwe tena nyumba ya Mungu. 14#Ezr 1:7,8; Hag 1:14 Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, alivyovitoa Nebukadneza katika hekalu lililokuwako Yerusalemu, na kuviingiza katika hekalu la Babeli, vyombo hivyo mfalme Koreshi alivitoa katika hekalu la Babeli, akakabidhiwa mtu, jina lake Sheshbaza, ambaye alikuwa amemfanya mtawala; 15naye akamwambia, Chukua vyombo hivi, uende, ukavitie katika hekalu lililoko Yerusalemu, na nyumba ya Mungu na ijengwe mahali pake. 16#Ezr 3:8,10; 6:15 Ndipo yule Sheshbaza alipokuja, akaupiga msingi wa nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na tangu wakati ule hadi leo imekuwa ikijengwa, wala bado haijamalizika. 17#Ezr 6:1,2; Mit 25:2 Basi, sasa, mfalme akiona vema, watu na wachunguze katika nyumba ya hazina ya mfalme, iliyoko huko Babeli, kama ni kweli ya kuwa mfalme Koreshi alitoa amri kuijenga nyumba hiyo ya Mungu katika Yerusalemu, na mfalme akatutumie habari ya mapenzi yake kuhusu jambo hili.

Iliyochaguliwa sasa

Ezra 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha