Kutoka 23:3-5
Kutoka 23:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini. “Ukimkuta ng'ombe au punda wa adui yako amepotea, utamrudishia mwenyewe. Ukimwona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, msaidie mtu huyo kumsimamisha punda wake, wala usimwache na kwenda zako.
Kutoka 23:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. Ukimwona ng'ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye akiwa ameanguka chini ya mzigo wake, na wewe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Kutoka 23:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. Ukimwona ng’ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Kutoka 23:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. “Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.