Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 23

23
Haki kwa wote
1 # Kut 20:16; Law 19:11-12; Kum 5:20; Mit 10:18; 1 Fal 21:10; Mit 19:5; Mdo 6:11 Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. 2#1 Fal 19:10; Ayu 31:34; Lk 23:23; Zab 72:2 Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; 3#Law 19:15 wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. 4#Kum 22:1-4; Mit 25:21; 1 The 5:15 Ukimwona ng'ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. 5Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye akiwa ameanguka chini ya mzigo wake, na wewe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
6 # Law 19:15; Kum 16:19; Ayu 31:13 Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. 7#Efe 4:25; Rum 1:18 Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu. 8#Mit 17:8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. 9#Zab 94:6; Kut 22:21; Law 19:33-34; Kum 24:17-18; 27:19 Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
Sheria kuhusu mwaka wa saba na Sabato
10 # Law 25:1-7 Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kupata mavuno yake; 11lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni. 12#Lk 13:14; Kut 20:9-11; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Kum 5:13-14 Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika. 13#Hos 2:17 Yaangalieni hayo yote niliyowaambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako.
Sikukuu za kila mwaka
14 # Kum 16:16 Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu. 15#Kut 12:14-20; Law 23:6-8; Hes 28:17-25 Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu; 16#Law 23:15-21,39-43; Hes 28:26-31 tena, sikukuu ya mavuno,#23:16 Kwingineko ni sikukuu ya vibanda. hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. 17Mara tatu katika mwaka wana wa kiume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.
18Usinitolee damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hadi asubuhi. 19#Kut 34:26; Kum 14:21; 26:2; Neh 10:35; Mit 3:9 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Kuahidiwa Ushindi juu ya Kanaani
20Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokuandalia. 21#Efe 4:30; Yos 24:19; 1 Yoh 5:16; Isa 9:6; Yer 23:6; Yn 10:38 Jitunzeni mbele yake, muisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22#Mwa 12:3 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23#Yos 24:8 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawatupilia mbali. 24#Kut 20:5 Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. 25#Kum 10:12; Yos 22:5; 1 Sam 2:20; Mt 4:10; Kum 7:15; 28:5 Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26#Ayu 21:10; Mwa 25:8 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. 27#Mwa 35:5; Kum 2:25; Yos 2:9,11; 1 Sam 14:15 Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuoneshe maungo yao. 28#Kum 7:20 Nami nitapeleka mavu#23:28 Maana si dhahiri neno hili lina maana ya ‘dondora’, maradhi mabaya au ‘baa’. mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. 29#Kum 7:22 Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa pori wakaongezeka na kukusumbua. 30Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. 31#1 Fal 4:21; Yos 21:44 Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako. 32Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao. 33#Kut 34:12,15; Kum 7:2; 12:30; Yos 23:13; Amu 2:3; 1 Sam 18:21; Zab 106:36,37 Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni (mtego) tanzi kwako.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 23: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha