Kumbukumbu la Sheria 11:16-17
Kumbukumbu la Sheria 11:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Jihadharini, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi yenu, akazifunga mbingu hata pasiwepo mvua na nchi ikaacha kutoa mazao yake, halafu mkaangamia upesi kutoka katika nchi nzuri ambayo Mwenyezi-Mungu anawapa.
Kumbukumbu la Sheria 11:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; hasira za BWANA zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo BWANA.
Kumbukumbu la Sheria 11:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; hasira za BWANA zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo BWANA.
Kumbukumbu la Sheria 11:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia. Ndipo hasira ya BWANA itawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayo BWANA anawapa.