Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 11

11
Thawabu za utiifu
1 # Zek 3:7 Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake. 2Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na watoto wenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka, 3#Kut 7:8—12:13 na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri; 4#Kut 14:28 na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi wao, na magari yao; na alivyowafunika kwa maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandama, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo; 5na mambo aliyowafanyia ninyi nyikani, hadi mkafika mahali hapa; 6#Hes 16:1,31-32; Zab 106:17 na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote; 7lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote. 8#Yos 1:6,7 Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi mwivukiayo kuimiliki; 9#Kum 4:40; 5:16; Mit 3:1,26; 10:27; Kut 3:8 nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali 10#Zek 14:18 Kwa kuwa nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinyunyizia maji kwa mguu wako, kama shamba la mboga; 11#Kum 8:7 lakini nchi muivukayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyunyizwa maji ya mvua ya mbinguni; 12#1 Fal 9:3 nayo ni nchi itunzwayo na BWANA, Mungu wako; macho ya BWANA Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.
13 # Law 26:3-5; Kum 7:12-16; 28:1-14; 6:17; 2 The 3:5 Tena itakuwa, mtakapoyazingatia kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, 14#Law 26:4; Kum 28:12; Yoe 2:23; Yak 5:7 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. 15#Zab 104:14; Yoe 2:19 Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba. 16#Ayu 31:27 Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; 17#Kum 6:15; 1 Fal 8:35; 2 Nya 6:26; 7:13 hasira za BWANA zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo BWANA. 18#Kum 6:6-9 Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. 19#Mit 22:6 Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 20#Hab 2:2 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; 21#Mit 3:2; 4:10; Zab 72:5; 89:29 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi. 22#Kum 6:17 Kwa kuwa kama mtayazingatia kwa bidii maagizo haya yote niwaagizayo, kuyafanya; kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kutembea katika njia zake zote, na kushikamana naye; 23#Kum 4:38; 9:1 ndipo BWANA atakapowafukuza mataifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuliko ninyi. 24#Yos 1:3-5; 14:9; Mwa 15:18; Kut 23:31; Hes 34:3 Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu. 25#Kum 7:24; Kut 23:27 Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu; BWANA, Mungu wenu, ataweka utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mtakayoikanyaga, kama alivyowaambia.
26 # Kum 30:1 Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; 27#Kum 28:2 baraka ni hapo mtakapoyafuata maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo; 28#Kum 28:15 na laana ni hapo msipotii maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkapotoka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
29 # Kum 27:11-14; Yos 8:33-35 Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali. 30Je! Haiwi ng'ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waishio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More? 31Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo. 32Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha