Kumbukumbu la Sheria 11:1-3
Kumbukumbu la Sheria 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kwa ajili hiyo, mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika siku zote kanuni zake, masharti yake, maagizo yake na amri zake. Fikirini kwa makini, kwa sababu ya watoto wenu ambao hawakujua wala hawakuona adhabu ya Mwenyezi-Mungu, uwezo wake na nguvu zake, ishara zake na maajabu yake aliyoyatenda kule Misri kwa Farao mfalme wa Misri na nchi yake yote
Kumbukumbu la Sheria 11:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake. Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na watoto wenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka, na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri
Kumbukumbu la Sheria 11:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake. Nanyi leo jueni; kwa kuwa sisemi sasa na vijana vyenu, ambao hawakujua, wala hawakuona adhabu ya BWANA, Mungu wenu, ukuu wake, na mkono wake wa nguvu, na mkono wake ulionyoka, na ishara zake, na kazi zake alizomfanya Farao mfalme wa Misri, na nchi yake yote, katikati ya Misri
Kumbukumbu la Sheria 11:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mpende BWANA Mungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote. Kumbuka hivi leo kwamba sio watoto wako walioona na kujua adhabu ya BWANA Mungu wako: utukufu wake, mkono wake wenye nguvu, mkono wake ulionyooshwa; ishara alizozifanya na mambo aliyoyafanya katikati ya Misri, kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote