Wakolosai 3:18-21
Wakolosai 3:18-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao. Enyi watoto, watiini wazazi wenu daima maana hiyo humpendeza Bwana. Nanyi wazazi, msiwachukize watoto wenu, la sivyo watakata tamaa.
Wakolosai 3:18-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Wakolosai 3:18-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Wakolosai 3:18-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.