Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kol 3

3
Maisha Mapya katika Kristo
1 # Zab 110:1; Kol 2:12 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2#Mt 6:33Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3#Rum 6:2Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4#1 Kor 15:43; Flp 1:21; Gal 2:20Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
5 # Rum 6:6; 8:13; Efe 4:19; 5:3,5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6#Efe 5:6kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. 7Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. 8#Efe 4:25-31; 5:4Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. 9#Efe 4:22Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; 10#Mwa 1:26; Efe 4:24mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. 11#Gal 3:28Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.
12 # Efe 4:2,32; 5:2; 1 Pet 2:9 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, 13#Efe 4:32; 5:2; Mt 6:14mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 14#Rum 13:8,10; Efe 4:3Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 15#Efe 4:4; Flp 4:7; 1 Kor 12:13,27Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 16#Efe 5:19-20Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 17#1 Kor 10:31; Efe 5:20Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Mawaidha kwa Familia
18 # Efe 5:22—6:9; 1 Pet 3:1 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. 19#Efe 5:25; 1 Pet 3:7Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. 20#Efe 6:1Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. 21#Efe 6:4Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa. 22#Efe 6:5-8Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana. 23Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, 24mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. 25#Kum 10:17; Rum 2:11; Efe 6:9Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Iliyochaguliwa sasa

Kol 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha