Matendo 27:22-23
Matendo 27:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini sasa ninawaombeni muwe na moyo; hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake; meli tu ndiyo itakayopotea. Kwa maana jana usiku malaika wa yule Mungu ambaye mimi ni wake na ambaye mimi ninamwabudu alinitokea
Matendo 27:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami
Matendo 27:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)