1 Wafalme 6:37-38
1 Wafalme 6:37-38 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika mwaka wa nne nyumba ya BWANA ilitiwa msingi, katika mwezi wa Zivu. Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
1 Wafalme 6:37-38 Biblia Habari Njema (BHN)
Msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu ulijengwa mnamo mwezi wa Zifu katika mwaka wa nne. Na katika mwezi wa Buli, yaani mwezi wa nane, katika mwaka wa kumi na mmoja, ujenzi wa nyumba ulimalizika, na kazi ilikuwa imekamilika kama ilivyopangwa. Ujenzi huo ulimchukua Solomoni miaka saba.
1 Wafalme 6:37-38 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika mwaka wa nne nyumba ya BWANA ilitiwa msingi, katika mwezi wa Zivu. Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
1 Wafalme 6:37-38 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Msingi wa Hekalu la BWANA uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano. Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba.