1 Mambo ya Nyakati 24:30-31
1 Mambo ya Nyakati 24:30-31 Biblia Habari Njema (BHN)
Mushi alikuwa na wana watatu: Mahli, Ederi na Yeremothi. Wao ni wazawa wa Lawi kulingana na koo zao. Pia hao wote walipiga kura kufuatana na ukoo wa kila mkuu na mdogo wake, kama wazawa wa Aroni walivyofanya. Walipiga kura mbele ya mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi.
1 Mambo ya Nyakati 24:30-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata koo za baba zao. Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.
1 Mambo ya Nyakati 24:30-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao. Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.
1 Mambo ya Nyakati 24:30-31 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi. Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.