Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 83

83
Sala ya hukumu juu ya adui wa Israeli
Wimbo. Zaburi ya Asafu.
1Ee Mungu, usistarehe,
Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.
2 # Zab 2:1 Maana adui zako wanafanya ghasia,
Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao.
3 # Zab 27:5; Kol 3:3 Juu ya watu wako wanafanya hila,
Na kushauriana juu yao uliowaficha.
4 # 2 Sam 10:6; 2 Nya 20:1 Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa,
Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
5Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,
Juu yako wanafanyana agano.
6Hema za Edomu, na Waishmaeli,
Na Moabu, na Wahagari,
7Gebali, na Amoni, na Amaleki,
Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,
8Ashuri naye amepatana nao,
Wamewasaidia wana wa Lutu.
9 # Hes 31:7,8; Isa 9:4; Amu 4:6-22; 7:1-23 Uwatende kama ulivyowatenda Midiani, Sisera,
Na Yabini, penye kijito cha Kishoni.
10Ambao waliangamizwa Endori;
Wakawa samadi juu ya nchi.
11 # Amu 7:25; 8:12 Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,
Na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
12Ambao Walisema,
Na tutamalaki makao ya Mungu.
13Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli,
Kama ya makapi mbele ya upepo,
14Kama moto uteketezao msitu,
Kama miali ya moto iiwashayo milima,
15Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako,
Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16Uzijaze nyuso zao fedheha;
Ili wapate kulitafuta jina lako, Ee BWANA.
17Waaibike, wafadhaike milele,
Naam, watahayarike na kupotea.
18Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA,
Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 83: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha