Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 4

4
1 # 2 Kor 1:14; 1 The 2:19,20 Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji langu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Mahimizo
2Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana. 3#Zab 69:28; Lk 10:20 Naam, nataka na wewe pia, mtumwa mwenzangu wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliofanya kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
4 # Flp 3:1; 2 Kor 13:11 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. 5#Ebr 10:37; Yak 5:8,9 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu. 6#Mt 6:25-34; Kol 4:2; 1 Pet 5:7; Zab 145:18; Yn 14:27 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7#Kol 3:15 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
8 # Rum 12:17 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo. 9#1 The 5:23; Rum 16:20; 1 Kor 14:33 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
Shukrani kwa zawadi za Wafilipi
10Nilifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi. 11#1 Tim 6:6 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo. 12#2 Kor 6:10 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. 13#2 Kor 12:10; 2 Tim 4:17 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. 14Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. 15#2 Kor 11:9 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. 16#Mdo 17:1 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. 17#1 Kor 9:11 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. 18#Kut 29:18; Eze 20:41; Flp 2:25 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. 19Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. 20Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
Salamu na baraka
21Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wanawasalimu. 22#Flp 1:13 Watakatifu wote wanawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari.
23Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

Iliyochaguliwa sasa

Wafilipi 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha