Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezra 4

4
Ujenzi wa hekalu wapingwa
1Basi adui za Yuda na Benyamini, waliposikia ya kuwa wana wa uhamisho wanamjengea BWANA, Mungu wa Israeli, hekalu, 2#Est 8:17; 2 Fal 17:24,32,33 wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa koo za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi tumemtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa. 3#Yn 4:9; Mdo 8:21; 2 Nya 36:22,23; Ezr 6:3; Isa 44:28 Lakini Zerubabeli, na Yoshua, na wakuu wengine wa koo za mababa katika Israeli, wakawaambia, Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba; bali sisi wenyewe peke yetu tutamjengea BWANA, Mungu wa Israeli, nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru. 4#Ezr 3:3; Isa 35:3,4; Yer 38:4 Ndipo wakazi wa nchi wakawavunja moyo watu wa Yuda, wakawafanya wawe na hofu ya kujenga. 5Wakawahonga maofisa, ili kuwakatisha tamaa katika mpango wao, siku zote za Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata wakati wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi.
Ujenzi wa Yerusalemu wapingwa
6Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu.
7Na tena, katika siku za Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzao wengine, wakimwandikia Artashasta, mfalme wa Uajemi, salamu za heri; na mwandiko wa waraka huo, ukaandikwa kwa herufi za Kiaramu, na kusomwa kwa lugha ya Kiaramu. 8#Zab 112:6; Zek 1:14; Rum 8:28 Nao Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, wakaandika waraka juu ya Yerusalemu kwa Artashasta, mfalme, kama hivi; 9#2 Fal 17:30,31 Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine, makadhi wa Kiajemi na madiwani wa Kiajemi; na Waarkewi, Wababeli, Washushani, yaani, Waelami; 10#Ezr 7:12 na watu wengine wa mataifa, ambao Asur-bani-pali mkuu, mwenye heshima, aliwavusha, na kuwakalisha katika mji wa Samaria, na mahali penginepo, ng'ambo ya Mto; na kadhalika.
11Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta;
Watumishi wako, watu walio ng'ambo ya Mto; wakadhalika. 12#Amo 7:10; Lk 23:2; Mdo 24:5 Ijulikane kwa mfalme ya kuwa Wayahudi, waliokwea kutoka kwako, wamefika kwetu Yerusalemu; nao wanaujenga ule mji mwasi, mbaya; wamemaliza kuta zake, na kuitengeneza misingi yake. 13#Ezr 7:24; Mt 9:9 Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara. 14Na sisi, kwa kuwa tunakula chumvi ya nyumba ya mfalme, wala si wajibu wetu kumwona mfalme akivunjiwa heshima, basi tumetuma watu na kumwarifu mfalme. 15#Est 3:8; Mdo 17:6,7 Ili habari zichunguzwe katika kitabu cha kumbukumbu za baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu cha kumbukumbu ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na wakuu wa mikoa, na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu mji huo ukaangamizwa. 16Tunamwarifu mfalme ya kuwa mji huo ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, basi utakuwa huna milki katika sehemu ya nchi iliyo ng'ambo ya mto.
17Ndipo mfalme akatuma majibu;
Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika. 18Ule barua mliotutumia umesomwa wazi mbele yangu, nami nikaielewa. 19Nikatoa amri, na watu wametafuta habari; ikaonekana ya kuwa mji huu zamani umewaasi wafalme, na ya kuwa uasi na fitina zimefanyika ndani yake. 20#1 Nya 18:3; Zab 72:8; Mwa 15:18 Tena walikuwako wafalme wakuu juu ya Yerusalemu, waliotawala nchi yote iliyo ng'ambo ya Mto; wakapewa kodi, na ada, na ushuru. 21Sasa toeni amri kuwakomesha watu hawa kazi yao, mji huu usijengwe, hadi nitakapotoa amri. 22Tena jihadharini, msilegee katika jambo hili; kwa nini madhara yazidi, na wafalme wapate hasara?
23 # Mit 4:16 Kisha nakala ya barua hiyo ya mfalme Artashasta iliposomwa mbele ya Rehumu, mtawala na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.
24 # Ayu 20:5 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu ikakoma; nayo ikakoma hadi mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi.

Iliyochaguliwa sasa

Ezra 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha