Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 3

3
Sifa za maaskofu
1 # Mdo 20:28 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu,#3:1 Askofu: maana yake ni, Mwangalizi. atamani kazi njema. 2#Tit 1:6-9 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha; 3asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha; 4#1 Sam 2:12 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 5(yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?) 6Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 7#1 Tim 5:10; 2 Kor 8:21; 1 Kor 5:12,13 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Sifa za mashemasi
8 # Flp 1:1; Mdo 6:3 Vivyo hivyo mashemasi#3:8 Shemasi: maana yake ni, Mtumishi wa kanisa. na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu; 9wakiishika siri ya imani kwa dhamiri safi. 10Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. 11#Tit 2:3 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; wasiwe wachongezi; ila wawe watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. 12Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. 13Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Siri ya dini yetu
14Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. 15#2 Tim 2:20; Efe 2:19-22 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16#Yn 1:14; 16:10; Rum 1:4; Mk 16:19 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.
Mungu alidhihirishwa katika mwili,
Akajulikana kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na malaika,
Akahubiriwa katika mataifa,
Akaaminiwa katika ulimwengu,
Akachukuliwa juu katika utukufu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha