Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 2

2
Maagizo kuhusu maombi
1 # Flp 4:6 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 3#1 Tim 1:1; 4:10 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 4#Eze 18:23; 2 Pet 3:9 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. 5#Rum 3:29,30; Ebr 12:24 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 6#Gal 1:4; 2:20; Tit 2:14 ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 7#2 Tim 1:11; Gal 2:7,8 Nami kwa ajili ya huo niliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
8Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 9#1 Pet 3:3-5 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10#1 Tim 5:10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11#Efe 5:22 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 12#1 Kor 14:34; Mwa 3:16 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe msikivu. 13#Mwa 1:27; 2:7,21-22; 1 Kor 11:8,9 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 14#Mwa 3:1-6; 2 Kor 11:3 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 15Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

Iliyochaguliwa sasa

1 Timotheo 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha