Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 103

103
Shukrani kwa Wema wa Mungu
Ya Daudi.
1Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
2Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 # Isa 33:24; Mt 9:2; Mk 2:5; Lk 7:47; Kut 15:26; Yer 17:14 Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
4Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema,
5Aushibisha mema uzee wako,
Ujana wako ukarejezwa kama tai;
6BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,
Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
7Alimjulisha Musa njia zake,
Wana wa Israeli matendo yake.
8 # Kut 34:6; Hes 14:18; Kum 5:10; Yak 5:11 BWANA amejaa huruma na neema,
Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
9 # Isa 57:16; Yer 3:5; Mik 7:18 Yeye hatateta sikuzote,
Wala hatashika hasira yake milele.
10 # Ezr 9:13 Hakututenda sawasawa na hatia zetu,
Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
11Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.
12 # Isa 43:25; Efe 1:7 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 # Kum 8:5; Isa 63:15,16; Mal 3:17 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.
14Kwa maana Yeye anatujua umbo letu,
Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.
15Mwanadamu siku zake zi kama majani;
Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.
16Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko!
Na mahali pake hapatalijua tena.
17 # Kut 20:6 Bali fadhili za BWANA zina wamchao
Tangu milele hata milele,
Na haki yake ina wana wa wana;
18 # Kum 7:9 Maana, wale walishikao agano lake,
Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.
19 # Zab 47:2 BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,
Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
20 # Mt 6:10 Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,
Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,
Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
21 # Mwa 32:2; Dan 7:9 Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote,
Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
22Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote,
Mahali pote pa milki yake.
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 103: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha