Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 102

102
Sala ya Kutaka Msaada kutoka kwa Mungu
Ombi la anayeteseka, akiwa hoi huku akimlilia BWANA.
1Ee BWANA, usikie kuomba kwangu,
Kilio changu kikufikie.
2Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,
Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
3 # Yak 4:14; Omb 1:13 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi,
Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
4Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka,
Naam, ninasahau kula chakula changu.
5Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu
Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu.
6 # Isa 34:11; Sef 2:14 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,
Na kufanana na bundi wa mahameni.
7Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro
Aliye peke yake juu ya nyumba.
8 # Mdo 23:12 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa;
Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu
Huapa kwa kunitaja mimi.
9Maana nimekula majivu kama chakula,
Na kukichanganya kinywaji changu na machozi.
10 # Zab 30:7 Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako;
Maana umeniinua na kunitupilia mbali.
11 # Yak 1:10 Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa,
Nami ninanyauka kama majani.
12 # 1 Tim 6:16 Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele,
Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
13 # Isa 40:2 Wewe mwenyewe utasimama,
Na kuirehemu Sayuni,
Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,
Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
14 # Dan 9:2 Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake,
Na kuyaonea huruma mavumbi yake.
15 # 1 Fal 8:43 Kisha mataifa wataliogopa jina la BWANA,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
16BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake,
17 # Neh 2:8 Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao.
18 # Rum 15:4; 1 Kor 10:11; Zab 22:31; Isa 43:21 Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu BWANA.
19 # Kum 26:15; Zab 14:2 Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi,
20Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
21Watu walitangaze jina la BWANA katika Sayuni,
Na sifa zake katika Yerusalemu,
22 # Hos 1:11 Pindi mataifa watapokusanyika pamoja,
Falme nazo ili kumtumikia BWANA.
23Amezipunguza nguvu zangu njiani;
Amezifupisha siku zangu.
24 # Zab 90:2; Hab 1:12; Ufu 1:4,8 Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu;
Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi.
25 # Mwa 1:1; Kut 20:11; Ayu 38:4-7; Ebr 1:10-12 Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi,
Na mbingu ni kazi ya mikono yako.
26 # Isa 66:22; Rum 8:20; 2 Pet 3:7 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu
Naam, hizi zitachakaa kama nguo;
Na kama mavazi utazibadilisha,
Nazo zitabadilika.
27 # Mal 3:6 Lakini Wewe U Yeye yule;
Na miaka yako haitakoma.
28Wana wa watumishi wako watakaa,
Na wazao wao wataimarishwa mbele zako.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 102: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha