Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ebr 2

2
Onyo kuhusu kuwa Makini
1Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. 2#Mdo 7:38,53; Gal 3:19Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, 3#Ebr 10:29; 12:25sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; 4#Mk 16:20; 1 Kor 12:4,11Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Kutukuka kwa Kujishusha
5Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
6 # Zab 8:4-6 Mwanadamu ni nini hata umkumbuke,
Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
7Umemfanya mdogo punde kuliko malaika,
Umemvika taji ya utukufu na heshima,
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
8 # 1 Kor 15:27 Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake.
Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake, 9#Flp 2:8,9ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. 10#Rum 11:36Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11#Mk 3:34,35; Mt 25:40; Yn 20:17Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; 12#Zab 22:22akisema,
Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu;
Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
13 # Isa 8:17,18; 2 Sam 22:3 Na tena,
Nitakuwa nimemtumaini yeye.
Na tena,
Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
14 # 2 Tim 1:10; Yn 12:31; Ufu 12:10; 1 Kor 15:56 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16#Isa 41:8,9Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17#Zab 22:22; Flp 2:7Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. 18#Ebr 4:15Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.

Iliyochaguliwa sasa

Ebr 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha