Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Efe 6

6
Watoto na Wazazi
1 # Kol 3:20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2#Kut 20:12; Kum 5:16Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. 4#Kol 3:21; Isa 50:5; Mit 2:2; 3:11; 19:18; Kum 6:7,20-25; Zab 78:4Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Watumwa na Mabwana
5 # Kol 3:22-25; Tit 2:9,10; 1 Pet 2:18 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; 6wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; 7kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; 8#2 Kor 5:10mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. 9#Kum 10:17; Kol 3:25; 4:1; 2 Nya 19:7; Mdo 10:34Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.
Silaha zote za Mungu
10 # 1 Kor 16:13; 1 Yoh 2:14 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11#Efe 4:14; 2 Kor 10:4Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12#Efe 2:2; Yn 14:30; Kol 1:13; 1 Pet 5:8,9Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13#1 Fal 20:11Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14#Isa 11:5; 59:17; Lk 12:35; 1 Pet 1:13; 1 The 5:8Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15#Isa 52:7; 40:3,9na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16#1 Pet 5:9; 1 Yoh 5:4zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17#Isa 59:17; 11:4; 49:2; 51:16; 1 The 5:8; Hos 6:5Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18#Mt 26:41; Kol 4:2,3kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 19#Kol 4:3; 2 The 3:1; Mdo 4:29pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; 20#2 Kor 5:20; Kol 4:4ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.
Mambo ya Kibinafsi na Baraka
21 # Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Kol 4:7 # Kol 4:7-8 Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote; 22#Kol 4:7,8ambaye nampeleka kwenu kwa kusudi lilo hilo mpate kuzijua habari zetu, naye awafariji mioyo yenu.
23Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. 24#1 Pet 1:8Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika.

Iliyochaguliwa sasa

Efe 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha