1
Efe 6:12
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Linganisha
Chunguza Efe 6:12
2
Efe 6:18
kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote
Chunguza Efe 6:18
3
Efe 6:11
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Chunguza Efe 6:11
4
Efe 6:13
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Chunguza Efe 6:13
5
Efe 6:16-17
zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu
Chunguza Efe 6:16-17
6
Efe 6:14-15
Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani
Chunguza Efe 6:14-15
7
Efe 6:10
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Chunguza Efe 6:10
8
Efe 6:2-3
Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
Chunguza Efe 6:2-3
9
Efe 6:1
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
Chunguza Efe 6:1
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video