Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kol 4

4
1 # Efe 6:9; Law 25:43,53 Ninyi akina bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Maagizo Zaidi
2 # 1 The 5:17; Efe 6:18; Flp 4:6 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; 3#Rum 15:30; Efe 6:18,19; 2 The 3:1; 1 Kor 16:9mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, 4#Efe 6:20ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. 5#Efe 5:15,16; 1 The 4:12Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6#Efe 4:29; Mk 9:50; 1 Pet 3:15Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Salamu za Mwisho na Baraka
7 # Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Efe 6:21 Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; 8#Efe 6:22ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu; 9#Flm 1:10-12pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.
10 # Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; 18:27; 19:29; 27:2; Flm 1:24 Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. 12#Kol 1:7; Flm 1:23Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu. 13Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli. 14#2 Tim 4:10,11; Flm 1:24Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu. 15Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. 16Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. 17#Flm 1:2Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.
18 # 1 Kor 16:21; 2 The 3:17 Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.

Iliyochaguliwa sasa

Kol 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha