Leseplan-informasjon

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 7 av 20

Katika sehemu hii, Luka anamtambulisha kamanda wa Kirumi, aitwaye Kornelio, anayewakilisha kila kitu ambacho Wayahudi walichukia kuhusu utawala wa Warumi. Malaika anamjia Kornelio na kumwambia amuite mtu anayeitwa Petro, anayeishi nyumbani kwa Simoni huko Yopa. Kornelio anapotuma wajumbe ili kufanya hilo, Petro yuko pale pale ambapo malaika alisema angekuwa, akishiriki katika maombi sambamba na tamaduni za Wayahudi, kisha ghafla anapata maono ya kushangaza. Katika maono, Mungu anamletea mkusanyiko wa wanyama ambao Wayahudi walikuwa wamekatazwa kula na kumwabia Petro, “kula hawa.” Petro anajibu, “Sijawahi kula kitu chochote kichafu.” Lakini Mungu anajibu, “usiite kichafu kile nilichokifanya kisafi.” Maono haya yanajirudia mara tatu na kumwacha Petro akiwa amekanganyika. Petro anavyoendelea kufikiri kuhusu maono hayo, wajumbe wanawasili wakiwa na mwaliko unaohitaji Petro asafiri nao ili kutembelea nyumba ya Kornelio. Tukio hili linamfanya Petro aanze kuelewa maono aliyoona. Petro anajua kuwa kuenda nyumbani kwa mtu asiye Myahudi kungepelekea hatari ya kujitia unajisi wa ibada, hivyo kwa hali ya kawaida angekataa mwaliko. Lakini kupitia maono, Mungu alimsaidia Petro kuona kuwa hafai kuita mtu yeyote najisi; Mungu ana uwezo wa kufanya safi watu wote wanaomtegemea Yesu. Hivyo bila kupinga, Petro anaenda nyumbani kwa Kornelio na kuwahubiria habari njema kuhusu Yesu––kifo chake, kufufuka na msamaha kwa wote wanaomwamini. Huku Petro akiendelea kuongea, Roho Mtakatifu anamshukia Kornelio na watu wote wa familia yake, kama tu alivyowafanyia wafuasi wa Kiyahudi wa Yesu katika siku ya Pentekoste! Vuguvugu linatawanyika ili kuwafikia watu wote, kama Yesu alivyosema ingefanyika. Soma, Tafakjari, kisha Ujibu: • Kabla ya kusoma vifungu vya leo, omba Mungu akupatie uelewa. Unatambua nini unavyotafakari unachokisoma? • Ni vikundi vipi vya watu ambavyo watu huona viko mbali na Mungu hawezi kuvifikia? Unafikiri ni kwa nini wana maoni hayo? Unafikiri soma la leo linawezaje kuathiri maoni yao? • Ruhusu kusoma kwako na kutafakari kwako kuchochee maombi. Mshukuru Mungu kwa kuwafikia wasio Wayahudi ili wawe sehemu ya familia yake. Muombe akusaidie ujiunge naye kwa njia zote ambazo upendo wake hujitoa kuwafundisha na kuwasamehe watu mbalimbali.
Dag 6Dag 8

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mih...

More

YouVersion bruker informasjonskapsler for å tilpasse opplevelsen din. Ved å bruke nettstedet vårt godtar du vår bruk av informasjonskapsler, som beskrevet i vår Personvernerklæring