Leseplan-informasjon

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumePrøve

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

Dag 9 av 20

Katika karne ya kwanza, watu wengi katiak eneo la Mediteraniani waliishi katika miji iliyojaa mno, yote ikitawaliwa na ufalme wa Kirumi. Kila jiji lilikuwa mchanganyiko wa tamaduni, makabila, na dini. Hivyo, kulikuwa na mahekalu tofauti tofauti ya kutoa kafara kwa miungu tofauti tofauti, na kila mtu alitiimiungu tofauti. Lakini, katika kila jiji ungepata vikundi vya watu wachache wasioabudu miungo hawa. Waisraeli, waliojulikana pia kama Wayahudi, walidai kuwa kulikuwa na Mungu mmoja wa kweli, na walitaka kumwabudu yeye pekee. Majiji haya yote yaliunganishwa kwa safu za barabara zilizojengwa na ufalme wa Kirumi, kwa hivyo ilikuwa rahisi kusafiri ili kufanya biashara na kueneza mawazo mapya. Mtume Paulo alitumia nusu ya pili ya maisha yake akisafiri katika barabara hizi, akitangaza kuwa Mungu wa Israeli alikuwa ameteua Mfalme mpya wa mataifa, ambaye hakutawala kwa nguvu wala ubabe bali kwa upendo wa kujitolea binafsi. Paulo alihudumu kama mbeba habari njema na aliwaalika watu wote kuishi chini ya utawala wa upendo wa Mfalme Yesu. Sehemu ya tatu ya Matendo ya Mitume inahusu simulizi za ziara za Paulo na jinsi watu walivyopokea ujumbe wake. Katika sehemu hii, Luka anatuonyesha jinsi Paulo na wafanyakazi wenzake walisafiri kutoka nyumbani kwao, katika jiji la Antiokia, hadi majiji yaliyopo maeneno ya kimkakati katika ufalme. Katika kila jiji, desturi ya Paulo ilikuwa kwenda Sinagogi la Kiyahudi kwanza ili kuwaonyesha watu wake jinsi Yesu alikuwa utimilifu wa kimasihi wa Biblia ya Kiebrania. Baadhi waliamini ujumbe wake na kuanza kuishi chini ya utawala wa Yesu, lakini wengine walipinga ujumbe wa Paulo. Baadhi ya Wayahudi waliona wivu na kuweka mashtaka ya uongo dhidi ya wanafunzi, huku baadhi ya wasio Wayahudi wakihisi kuwa njia yao ya maisha ya Kirumi ilikuwa inatishiwa na kuwafukuza wanafunzi. Lakini upinzani kamwe haukukomesha vuguvugu la Yesu. Kusema kweli, kutenswa kwao kulisaidia kuieneza injili majiji mapya. Wakiwa wamejawa furaha na Roho Mtakatifu, wanafunzi waliendelea kujikaza. Soma, Tafakari, kisha Ujibu: •Pitia ujumbe wa Paulo kwa makini (tazama Matendo ya Mitume 13:40). Tambua ni simulizi zipi za Agano la Kale, maelezo, na nukuu alizochagua kutaja ili kuonyesha kuwa Yesu ndiye Mfalme ambaye Israeli ilikuwa inamsubiri. Unatambua nini? • Umewahi kuona wivu pale mtu mwingine anapoteka fikra za watu kwa sababu ya jinsi anavyotumia kipaji chake na kumfuata Yesu? Pitia majibu ya baadhi ya viongozi wa dini (tazama 13:42-50) na jibu la wanafunzi (tazama 13:51-52). Hili linakutia moyo au kukupatia changamoto vipi leo? • Yesu amedhamiria kuleta umoja, lakini anajua kuwa ujumbe wake utakataliwa vikali na baadhi ya watu, hivyo anawaelekeza wanafunzi wake inavyofaa. Pitia somo la leo ukiangazia toleo la kwanza la Luka lililonukuu maneno ya Yesu (tazama Luka 10:5-16). Unatambua nini? • Nakili Matendo ya Mitume 13:38-39 kwa mwandiko wako na kisha weka nakala hiyo mahali ambapo utaiona wiki nzima. Yesu anatoa msamaha kamilifu na uhuru kwa njia ambazo agano la kale halikuweza. Kuna kitu kingine nje ya Yesu ambacho huwa unakitazamia kwa msaada, tumaini na uhuru? Ongea na Mungu kuhusu hilo sasa. Muombe akusaidie kumuona na kumheshimu kama Mfalme mmoja tu wa kweli katika maisha yako.
Dag 8Dag 10

Om denne planen

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mih...

More

YouVersion bruker informasjonskapsler for å tilpasse opplevelsen din. Ved å bruke nettstedet vårt godtar du vår bruk av informasjonskapsler, som beskrevet i vår Personvernerklæring