YouVersion Logo
Search Icon

Wimbo Ulio Bora 7

7
Bwana arusi
1Nyayo zako katika viatu zapendeza sana!
Ewe mwanamwali wa kifalme.
Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,
kazi ya msanii hodari.
2Kitovu chako ni kama bakuli
lisilokosa divai iliyokolezwa.
Tumbo lako ni kama lundo la ngano
lililozungushiwa yungiyungi kandokando.
3Matiti yako ni kama paa mapacha,
ni kama swala wawili.
4Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu;
macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni,
karibu na mlango wa Beth-rabi.
Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,
ambao unauelekea mji wa Damasko.
5Kichwa chako juu yako ni kama mlima Karmeli,
nywele zako za ukoka zangaa kama zambarau;
uzuri#7:5 uzuri: Kiebrania si dhahiri. wako waweza kumteka hata mfalme.
6Tazama ulivyo mzuri na wa kuvutia!
Ewe mpenzi, mwali upendezaye!
7Umbo lako lapendeza kama mtende,
matiti yako ni kama shada za tende.
8Nilisema nitaupanda mtende na kuzichuma shada za tende.
Kwangu matiti yako ni kama shada za zabibu,
harufu nzuri ya pumzi yako ni kama matofaa;
9na kinywa chako ni kama divai tamu.
Bibi arusi
Basi divai na itiririke hadi kwa mpenzi wangu,
ipite juu ya midomo yake na meno yake!#8:9 midomo yake na meno yake: Kiebrania: Midomo ya wale walalao.
10Mimi ni wake mpenzi wangu,
naye anionea sana shauku.
11Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani,
twende zetu tukalale huko vijijini.
12Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu,
tukaone kama imeanza kuchipua,
na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua,
pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua.
Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.
13Harufu nzuri ya tunguja imejaa hewani
karibu na milango yetu kuna kila aina ya matunda bora,
yote mapya na ya siku za nyuma,
ambayo nimekuwekea wewe mpenzi wangu.

Currently Selected:

Wimbo Ulio Bora 7: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy