YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 80

80
Maombi kwa ajili ya taifa
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yungiyungi. Zaburi ya Asafu)
1Utege sikio, ewe Mchungaji wa Israeli,
uwaongozaye wazawa wa Yosefu kama kondoo.
Ewe ukaaye juu ya viumbe vyenye mabawa,#80:1 viumbe vyenye mabawa: Taz maelezo ya Mwa. 3:24 uangaze,
2mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.
Uoneshe nguvu yako, uje kutuokoa!
3Uturekebishe, ee Mungu;
utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka.
4Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi,
hata lini utazikasirikia sala za watu wako?
5Umefanya huzuni iwe chakula chetu;
umetunywesha machozi kwa wingi.
6Umetufanya tuwe dharau kwa jirani zetu;
maadui zetu wanatudhihaki.
7Ee Mungu wa majeshi, uturekebishe,
utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka.
8Ulileta mzabibu kutoka Misri;
ukawafukuza watu wa mataifa mengine,
na kuupanda katika nchi yao.
9Uliupalilia upate kukua,
nao ukatoa mizizi na kuenea kote nchini.
10Uliifunika milima kwa kivuli chake,
na matawi yake yakawa kama mierezi mikubwa.
11Matawi yake yalienea mpaka baharini;
machipukizi yake mpaka kando ya mto Eufrate.
12Mbona ulibomoa kuta zilizouzunguka?
Sasa kila apitaye anachuma zabibu zake;
13nguruwe mwitu wanauharibu,
na wanyama wa porini wanautafuna!
14Utugeukie tena ee Mungu wa majeshi.
Uangalie toka mbinguni, uone;
ukautunze mzabibu huo.
15Uulinde mche ulioupanda kwa mkono wako;
hilo chipukizi uliloimarisha wewe mwenyewe.
16Watu walioukata na kuuteketeza,
uwatazame kwa ukali, waangamie.
17Mkono wako umkinge huyo uliyemfadhili;
huyo uliyemteua kwa ajili yako.
18Hatutakuacha na kukuasi tena;
utujalie uhai, nasi tutakusifu.
19Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi uturekebishe;
utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka.

Currently Selected:

Zaburi 80: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy