YouVersion Logo
Search Icon

Hosea 7

7
1Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu,
ninapotaka kuwaponya Waisraeli,
uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa,
matendo mabaya ya Samaria hujitokeza.
Wao huongozwa na udanganyifu,
kwenye nyumba wezi huvunja
nje barabarani wanyang'anyi huvamia.
2Hawafikiri hata kidogo kwamba mimi
nayakumbuka maovu yao yote.
Sasa maovu yao yamewabana.
Yote waliyotenda yako mbele yangu.
Uhaini katika ikulu
3“Wanamfurahisha mfalme kwa maovu yao
wanawafurahisha wakuu kwa uhaini wao.
4Wote ni wazinzi;
wao ni kama tanuri iliyowashwa moto
ambao mwokaji hauchochei tangu akande unga
mpaka mkate utakapoumuka.
5Kwenye sikukuu ya mfalme,
waliwalewesha sana maofisa wake;
naye mfalme akashirikiana na wahuni.
6Kama tanuri iwakavyo,
mioyo yao huwaka kwa hila;
usiku kucha hasira yao hufuka moshi,
ifikapo asubuhi, hulipuka kama miali ya moto.
7Wote wamewaka hasira kama tanuri,
na wanawaangamiza watawala wao.
Wafalme wao wote wameanguka,
wala hakuna anayeniomba msaada.
Israeli anategemea mataifa mengine
8“Efraimu amechanganyika na watu wa mataifa.
Anaonekana kama mkate ambao haukugeuzwa.
9Wageni wamezinyonya nguvu zake,
wala yeye mwenyewe hajui;
mvi zimetapakaa kichwani mwake,
lakini mwenyewe hana habari.
10Kiburi cha Waisraeli chashuhudia dhidi yao,
hawanirudii mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao;
wala hawanitafuti kwa matukio hayo yote.
11Efraimu ni kama njiwa, mjinga asiye na akili;
mara yuko Misri, mara Ashuru kuomba.
12Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase,
nitawaangusha chini kama ndege wa angani;
nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.
13Ole wao kwa kuwa wameniacha!
Maangamizi na yawapate, maana wameniasi.
Nilitaka kuwakomboa,
lakini wanazua uongo dhidi yangu.
14“Wananililia, lakini si kwa moyo.
Wanagaagaa na kujikatakata vitandani mwao,
kusudi nisikilize dua zao za nafaka na divai;
lakini wanabaki waasi dhidi yangu.
15Mimi ndimi niliyeiimarisha mikono yao,
lakini wanafikiria maovu dhidi yangu.
16Wanaigeukia miungu batili,
wako kama uta uliolegea.
Viongozi wao watakufa kwa upanga,
kwa sababu ya maneno yao ya kiburi.
Kwa hiyo, watadharauliwa nchini Misri.

Currently Selected:

Hosea 7: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy