YouVersion Logo
Search Icon

Hosea 5

5
Wakufunzi wabaya wa Israeli
1“Haya! Sikilizeni enyi makuhani!
Tegeni sikio, enyi Waisraeli!
Sikilizeni enyi ukoo wa kifalme!
Nyinyi mlipaswa kuzingatia haki,
badala yake mmekuwa mtego huko Mizpa,
mmekuwa wavu wa kuwanasa huko Tabori.
2Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu.
Lakini mimi nitawaadhibuni nyote.
3Nawajua watu wa Efraimu,
Waisraeli hawakufichika kwangu.
Nyinyi watu wa Efraimu mmefanya uzinzi,
watu wote wa Israeli wamejitia najisi.
Hosea aonya dhidi ya ibada za miungu
4“Matendo yao yanawazuia wasimrudie Mungu wao.
Mioyoni mwao wamejaa uzinzi;
hawanijui mimi Mwenyezi-Mungu.
5Kiburi cha Waisraeli chaonekana wazi;
watu wa Efraimu watajikwaa katika hatia yao,
nao watu wa Yuda watajikwaa pamoja nao.
6Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng'ombe,
kumtafuta Mwenyezi-Mungu;
lakini hawataweza kumpata,
kwa sababu amejitenga nao.
7Wamevunja uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu,
wamezaa watoto walio haramu.
Mwezi mwandamo utawaangamiza,
pamoja na mashamba yao.
Vita kati ya Yuda na Israeli
8“Pigeni baragumu huko Gibea,
na tarumbeta huko Rama.
Pigeni king'ora huko Beth-aveni.
Enyi watu wa Benyamini, adui yenu yuko nyuma!
9Siku nitakapotoa adhabu
Efraimu itakuwa kama jangwa!
Ninachotangaza miongoni mwa makabila ya Israeli,
ni jambo litakalotukia kwa hakika.
10Viongozi wa Yuda wamekuwa
wenye kubadili mipaka ya ardhi.
Mimi nitawamwagia hasira yangu kama maji.
11Efraimu ameteswa,
haki zake zimetwaliwa;
kwani alipania kufuata upuuzi.
12Hivyo mimi Mungu niko kama nondo kwa Efraimu,
kama donda baya kwa watu wa Yuda.
13Watu wa Efraimu walipogundua ugonjwa wao,
naam, watu wa Yuda walipogundua donda lao,
watu wa Efraimu walikwenda Ashuru
kuomba msaada kwa mfalme mkuu;
lakini yeye hakuweza kuwatibu,
hakuweza kuponya donda lenu.
14Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu,
kama mwanasimba kwa watu wa Yuda.
Mimi mwenyewe nitawararua na kuondoka,
nitawachukua na hakuna atakayewaokoa.
15Nitarudi mahali pangu na kujitenga nao
mpaka wakiri kosa lao na kunirudia.
Taabu zao zitawafundisha wanitafute, wakisema:

Currently Selected:

Hosea 5: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy