YouVersion Logo
Search Icon

Zab 145

145
Ukuu na Wema wa Mungu
Sifa. Ya Daudi.
1Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
3BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani.
4Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,
Kitayatangaza matendo yako makuu.
5Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,
Na matendo yako yote ya ajabu.
6Watu watayataja matendo yako ya kutisha,
Nami nitausimulia ukuu wako.
7Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.
Wataiimba haki yako.
8 # Kut 34:6; Hes 14:18; Zab 86:5,15; 57:10; Omb 3:22,23; Yn 1:17 BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9 # Zab 100:5; Nah 1:7; Mt 5:45; Mdo 14:17 BWANA ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
10 # Zab 19:1 Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
12Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14BWANA huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.
15Macho ya watu wote yakuelekea Wewe,
Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16Waufumbua mkono wako,
Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
18 # Zab 91:1; Isa 61:10; Yn 14:23; Yak 4:8; 1 Yoh 2:24; Yud 1:23; Ufu 3:20; Yn 4:24 BWANA yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 # 1 Yoh 5:14 Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
20 # 1 Pet 1:5 BWANA huwahifadhi wote wampendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza.
21Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
milele na milele.

Currently Selected:

Zab 145: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy