YouVersion Logo
Search Icon

Zab 144

144
Sala kwa Ukombozi wa Kitaifa na Usalama
Ya Daudi.
1 # 2 Sam 22:35 Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,
Anifundishaye mikono yangu vita,
Vidole vyangu kupigana.
2Mhisani wangu na boma langu,
Ngome yangu na mwokozi wangu,
Ngao yangu niliyemkimbilia,
Huwatiisha watu wangu chini yangu.
3 # Ayu 7:17-18; Zab 8:4; Ebr 2:6 Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue?
Na binadamu hata umwangalie?
4Binadamu amefanana na ubatili,
Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
5 # Isa 64:1 BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke,
Uiguse milima nayo itatoka moshi.
6Utupe umeme, uwatawanye,
Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
7 # Zab 69:1; Mal 2:11 Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,
Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
8Vinywa vyao vyasema visivyofaa,
Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
9 # Zab 33:2 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
10Awapaye wafalme wokovu,
Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
11Uniponye, unitoe,
Katika mkono wa wageni.
Vinywa vyao vyasema visivyofaa,
Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
12Wana wetu na wawe kama miche
Waliokua ujanani.
Binti zetu kama nguzo za pembeni
Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
13Ghala zetu na zijae
Zenye akiba za jinsi zote.
Kondoo zetu na wazae
Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
14 # Law 26:17 Ng’ombe zetu na wachukue mizigo,
Kusiwe na kushambuliwa.
Wala kusiwe na kuhamishwa,
Wala malalamiko katika njia zetu.
15 # Kum 33:29 Heri watu wenye hali hiyo,
Heri watu wenye BWANA kuwa Mungu wao.

Currently Selected:

Zab 144: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy