Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Muda wa kupumua Mfano

Breathing Room

SIKU 5 YA 5

Ninakiri kwamba mwenye kufurahisha watu. (Wewe pia?) Lakini nimegundua kwamba jina hilo si kamili. Kuwa mwenye kufurahisha watu pia ni kuwa mwenye kusikitisha watu. Kubaki ofisini mpaka usiku ili kumfurahisha mkubwa wako ni kumsikitisha unayefanya mazoezi ya viungo naye kwani hutaenda kujiunga naye. Kujiunga na klabu ya kujadiliana kuhusu vitabu ili kufurahisha marafiki zako ni kusikitisha mume/mke wako kwani hutajiunga naye kukula chajio. Unaona? Kila ndio kumfurahisha mtu pia ni la ambayo inamsikitisha mtu mwengine.


Kama wewe ni kama mimi, unajaribu kufurahisha kila mtu kwa hivyo unapoteza muda wako wa kupumua kwani unataka kufanya kila kitu. Nitakula chajio nyumbani kisha nitachelewa kidogo kwa mkutano wa klabu ya vitabu! 


Tunapomaliza somo letu la muda wetu wa kupumua, ningependa kukuelekeza kwa hadithi moja katika Agano la Kale—hasa mstari mmoja—ambao ulibadilisha msimu mmoja wa maisha yangu. Miaka na mikaka kabla ya Yesu, mji wa Yerusalemu ulikuwa umeshambuliwa na kubomolewa. Kujenga upya kuta za mji kulikuwa muhimu, na kiongozi alikuwa Nehemia. Siku moja, alipata mwaliko, na jibu lake ikawa mstari muhimu kwangu. Nehemia alisema, “…Ninafanya kazi muhimu, na siwezi kuja kwako. Mbona kazi ikome ninapoiacha kuja kwako?”


Wakati ambapo niliusikia mstari huu kwa mara ya kwanza, nilikuwa na watoto watatu nyumbani ambao walikuwa wadogo, nilikuwa namfunza mkubwa wao nyumbani, na mume wangu alikuwa akizindua kanisa. Hatukuwa na muda wa kupumua. Hata hivyo, ilikuwa ngumu kwangu kukataa nafasi na mialiko nilizopata.


Nilipewa ruhusa kupa watu muhimu kipaumbele katika maisha yangu kutoka maneno haya ya Nehemia. Kuwa mama ilikuwa “kazi yangu muhimu.” Sikuweza kujiunga na jopo hilo au kuzungumza katika hafla hiyo ya wanawake. Kusema ndio kwa vitu hivi ungekuwa sawa na kusema la kwa “kazi yangu muhimu” kwa familia yangu. 


Kina dada, tunaweza kujitolea, wakati wetu, pesa yetu, na muda wetu wa kupumua mpaka kilichobaki kwa wapendwa wetu ni makombo. Badala yake, turudishe muda wetu wa kupumua kwa kuwapa wapendwa wetu kipaumbele. Na kwa mambo mengine, tutasema, “Ninafanya kazi muhimu na siwezi kuja kwako.”


Ikiwa ulipendezwa na mpango huu, tazama somo la video lenye sehemu nne ambako mpango huu ulitolewa kwa kupakua apu ya Breathing Room Devotional ni bure


Andiko

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Breathing Room

Unahisi kana kwamba hufurahi chochote kwa sababu unajaribu kufanya kila kitu? Unafanya mambo mengi kwa wakati mmoja katika maisha yako na wapendwa... Wewe ni mfanisi. Lakini umechoka tiki. Unahitaji tu muda kidogo kupumu...

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Sandra Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://breathingroom.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha