Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 4 YA 14

Kuelewa na kufurahia sauti ya Mungu imekuwa ni safari ya kufurahisha sana ya maisha yangu. Sauti yake inaleta umuhimu wake na kumbatio lake. Anapozungumza, ananitetemesha kwa sauti yake. Kwa hiyo kuielewa sauti yake ni kukutana na Yeye.



Uzoefu umethibitisha kwamba sikuhofia kwamba Yesu atasema kwa sababu sauti yake inaleta uwepo wake, na utu wake siku zote ni mpole--hata kama anaonya. Anaheshimu kama Bwana harusi anavyomheshimu Bibi harusi. Uzuri wake usiobadirika unanifundisha kumwamini. 



Alama yangu ya kwanza kwamba Bwana anaongea ni kwamba sauti yake inatuliza usikivu wangu. Wakati mwingine mawasiliano yake huwezi kuyachanganya. Lakini maneno yake wakati mwingine yanaweza kudhaniwa ni mawazo yangu na fikra zangu au ni maneno ya wanaonizunguka. Ndipo nashangaa, " Ni Bwana anaongea au ninaongozwa na akili yangu, mapenzi yangu na hisia zangu?" 



Nilimuuliza Bwana mara moja juu ya mashaka ya kutambua sauti yake. Alichonifunulia kilinishangaza. Alisema asilimia tisini ya muda nilipoacha kushangaa kama alikuwa anaongea, ilikuwa hakika ni sauti yake. Ndipo nikatishika zaidi kwa sababu mara nyingi nilipuuzia sauti yake na kupelekea kuwa mkaidi. Sheria yangu: Kama nitasimama na kuuliza, " Huyu ni Bwana?"--yawezekana ni Mungu! Ufunuo wa jinsi ya kuendelea unafuata na kukubali kwamba kweli anaongea.



Sasa ninatamani mawasiliano na Bwana. Mawazo yake ni hekima safi, tofauti na asili ya mawazo yangu. Anapozungumza, huleta ukweli na kupanua ufinyu wa ufahamu wangu kwa ushauri wake. Katikati ya ufunuo wake wa kimwili na maelekezo yake, mara nyingi nakuta uelewa wangu umehama pasipo kutarajia muda huohuo nakua sijui, sielewi; mara ninajua jambo kwa uhakika na kwa hiari najikuta nasema, "Oh! Sasa ninaelewa."



Kadri roho yangu inavyoelewa mawasiliano yake na uwepo wake, amani mara nyingi huingia na kutawanyika, au furaha hububujika kutoka ndani. Machozi yasiyozuilika hufuata. Nadhani ni wema wake ambao huamsha mwitikio katika viwango vingi. Sauti yake huleta mwitikio--ambao unakuwa ni somo la maongezi yetu yanayofuata.


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta t...

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha