Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano

Killing Kryptonite With John Bevere

SIKU 1 YA 7


Pengine itakushangaza kwamba lengo langu la siku ya kwanza ya ibada hii ni kukuvuruga . . . nitakuambia kwa nini.


Pana utengano mkubwa kati ya yaliyofanyika katika kanisa la Agano Jipya na yanayofanyika katika kanisa la leo. Ingekuwa rahisi kusema kwamba tofauti hii inatokana na taasisi zisizo na muungano, viongozi wasiomcha Mungu, utamaduni, na kadhalika, lakini tutumie fursa hii kutathmini maisha yetu wenyewe. 


Ukweli ni kwamba, Wakristo wa karne ya kwanza walikuwa si
wanadamu wa kawaida katika siku hizo, na ulimwengu uliwashangaa. Ifuatayo ni mifano michache tu ya vitendo vikuu vinavyopatikana katika Maandiko:


Hakuna mtu katika jamii zao aliyekosa chochote—hakuna aliyekuwa na mahitaji ya kimwili ya aina yeyote, hakuna aliyetegemea msaada kutoka serikalini (Matendo 4:33–35). Kwa muda mfupi miji yote ikaja kwa Yesu, na injili ikaenea katika maeneo yote katika miaka michache (Matendo 9:32–35, 19:10). 


Nguvu ya Mungu ilitenda kazi Kupitia kwao sana hadi walilazimika kushawishi watu kuwa hawakuwa miungu (Matendo 10:25–26, 14:8–18)—fikiria kuhusu hilo kwa sekunde chache. Walikuwa na ibada ya nguvu sana mpaka ardhi ilitikisika (Matendo 4:31). Na kwa sababu ya hayo, walikuwa na sifa ya kuwa watu walioupindua ulimwengu (Matendo 17:6). 


Kinachofaa kutupa changamoto sana ni kwamba Mungu anafanya dhahiri katika Neno lake kwamba Wakristo wa siku za mwisho wangefanya hata zaidi ya hao waumini wa kwanza. Swali ni, mbona hatuoni matendo makuu zaidi ambayo Mungu aliahidi?


Naamini kwamba kama vile Superman alikuwa na "nguvu ya kubadilisha", kanisa—jumla ya mtu mmoja mmoja ambao wanadai kumfuata Kristo—wanaweza pia. 


"Nguvu ya kubadilisha" ni kitu kinachotoka katika sayari ya Superman ambayo ni nyumbani kwake. Alipoikaribia, angepoteza nguvu zake za kipekee na kuwa dhaifu—hata kuwa dhaifu kuliko mtu wa kawaida. Ukitazama kanisa la leo—kiwango cha talaka, matumizi ya ponografia, na uasherati ni vya juu au juu sana kuliko Vya ulimwengu—ni wazi kwamba tuna nguvu ya kubadilisha kati yetu. 


Hali ya kanisa la leo, ambayo inatofautiana sana na makusudio na nia za Mungu kwa maisha yetu kama wafuasi wa Kristo, inafaa kukuchanganya. 


Katika ibada hizi, tutajifunza nguvu hii ni nini na jinsi ya kuiondoa, lakini kwanza lazima tujue na tuamini uwezo wetu. Hutakuwa na motisha kutumia uwezo wako ambao huujui. 


Utafanya nini sasa baada ya kujua uwezo wako? 


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Killing Kryptonite With John Bevere

Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango hu...

More

Tungependa kumshukuru John na Lisa Bevere (Messenger Int'l) kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://killingkryptonite.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha