Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

MsihangaikeMfano

Msihangaike

SIKU 4 YA 5

Wokovu Wetu Kutokana na Wasiwasi/Kuhangaika

Katika msitari wa 33, maneno ya Kristo yanaweza kufupishwa hivi: Acheni imani yenu kwa Mungu iwe jambo kuu zaidi maishani mwenu, kumtii Mungu, ambaye ndiye Baba yenu wa mbinguni. Amewaleta na kuwaweka katika ufalme wake. Kwa hivyo, msimamo wenu mwema kupitia imani ndani ya Kristo uonekane maishani mwenu kila siku mnapoendelea kumtegemea kwa mahitaji yenu yote.

Mapema katika msitari wa 8 katika sura hii, Kristo alisema: Baba yenu anajua mnayohitaji kabla hamjamuomba. Katika mstari wa 25 na 27, Kristo anauliza maswali haya: Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongezea hata saa limoja kwa uhai wake? Basi hivyo katika msitari wa 34, Kristo anamalizia kwa kusema hivi: Basi, msisumbukie ya kesho kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Kila siku yatosha kwa maovu yake.

Huwa tunafikiri eti wasiwasi ni tukio bila hiari yetu na hatuwezi kudhibiti au kufanya lolote ili kuzuia hali hiyo. Lakini, katika kifungu hiki, tunaona ya kwamba siyo hivyo kabisa, la sivyo, Kristo hangetuamuru tusihangaike.

Kwa kutoa amri hiyo tusiwe na wasiwasi, Kristo anatusaidia kufahamu kuwa wasiwasi ni chaguo letu la kuhangaikia hali zetu na kulingana na mtazamo wetu kuhusu Mungu, fedha, na mali zetu.

Hivyo, katika kifungu hiki, Kristo anasema, kama utaruhusu Injili ibadili mtazamo wako, utaacha kuhangaika kwa sababu utajua kwa dhati kwamba Baba yako wa Mbinguni, aliyemtoa Kristo kwa ajili yako msalabani, atatosheleza mahitaji yako yote ya kila siku (Warumi 8:32).

Kwa ufupi, Kristo aliwaambia watu hawa, nasi pia leo: Acheni wasiwasi na kuhangaikia maisha yenu kila siku kwa sababu Mungu, Baba yenu wa Mbinguni, amekwisha kuyashughulikia mahitaji ya maisha yenu ya leo, kesho, na siku zote zijazo! Acheni Wasiwasi! Msihangaike!

Basi, tunaweza kusema mhtasari wa somo hili la tatu, katika kifungu hiki, unasema kuwa injili inatuokoa kutokana na mahangaiko tunapotazama jinsi Mungu alivyotutendea msalabani, kwa sababu injili inatuwezesha kubadili imani yetu kutoka kwa fedha na kuiweka kwa Mungu, na aliyotutendea kupitia kwa Kristo.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Msihangaike

Katika kitabu cha Mathayo 6:24-34 Kristo anaeleza jinsi Injili inadhihirisha sababu hasa tunakumbwa na wasiwasi au mahangaiko, na la muhimu zaidi, Kristo anatuwezesha kuelewa jinsi Injili inavyotuokoa kutokana na uwepo w...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha