Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Tumaini, Jibidishe, Na PumzikaMfano

Trust, Hustle, And Rest

SIKU 1 YA 4

Tumaini, Jibidishe, na Pumzika


“Jibidishe” ni lazima litakuwa moja ya maneno maarufu katika biashara leo. Tanki la nyangumi wawekezaji huwasukuma wajasiliamali ili kuongeza mauzo. Kila mmoja anaonekana "anajibidisha upande wake" akiwa na kazi 9-5. Lakini Biblia inasema nini juu ya kujibidisha kwetu? Kwa upande mmoja, Maandiko yanasifia kufanya kazi kwa bidii. Wakolosai 3:23 inatuagiza “Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo.” Lakini wakati wakristo wanaweza kujiunga katika kushangilia desturi ya kufanya kazi kwa bidii, lazima tupambane na kweli ya Biblia kwamba ni Mungu, siyo sisi au jitihada zetu, zinazozaa matunda (Kumbu Kumbu la Torati 8:17-18). Kama wakristo, lazima tukubali mvutano kati ya kufanya kazi kwa bidii na kumtumaini Mungu ili kupata pumziko la kweli.


Yoshua 6 inatoa mfano mzuri sana wa jinsi inavyoonekana kukubali mvutano vizuri. Wakati wana wa Israeli walikuwa wanaongozwa na Yoshua kwenda nchi ya ahadi, walikumbana na kikwazo kikubwa: kilichoonekana hakiwezekani mji wa Yeriko. Kama Yoshua 6:2 inavyoandikwa, Bwana akamwambia Yoshua, tazama, nimeutia Yeriko mkononi mwako," lakini badala ya kumpa Yoshua na wana wa Israeli nguvu za kimungu na uwezo wa kuuchukua Yeriko wao wenyewe, Mungu aliwataka waweke tumaini lao lote kwake. Mungu alimwagiza Yoshua kuwaongoza wana wa Israeli katika kuuzunguka mji wa Yeriko siku saba, wakimalizia kwa kupiga kelele kwa sauti kuu.  


Kama nyakati nyingi katika historia, Mungu alichagua kutumia " vitu vya kijinga vya dunia hii kuaibisha wenye hekima." Kuliko kuwaruhusu Yoshua na wana wa Israeli kushinda vita kwa nguvu zao wenyewe, Mungu aliweka mpango kuhakikisha kwamba yeye peke yake atatukuzwa. Kabla ya kuwapa wana wa Israeli ushindi, Mungu aliwataka kumtumaini kuwashindia. Pasipo kupepesa macho, Yoshua alifanya hivyo. Wana wa Israeli waliuamini mpango wa Mungu. Ndipo, walijibidisha: wakazunguka, wakipiga matarumbeta yao, na kupiga kelele mpaka kuta za Yeriko zikaanguka.  


Ni wazi, haikuwa ni kuzunguka kwa wana wa Israeli, kupiga kelele, na kujibidisha kuliko ziangusha kuta za Yeriko. Ilikuwa ni Mungu. Na hicho ndicho nafikiria Mungu alitaka wana wa Israeli na sisi kuona. Juhudi zetu za kazi ni jambo jema! Lakini kuamini kwamba juhudi zetu ndizo zinaleta matokeo katika kazi zetu itakuwa sawa na wana wa Israeli kuamini kwamba kupiga kelele kulileta kuta zisizopenyeka kuanguka chini.


Kama Yoshua na wana wa Israeli wanavyotuonesha, haitupasi kutafuta kuondoa mvutano kati ya kuamini na kujibidisha; badala yake, yatupasa kukubali. Mawazo hayo hayapingani, yamekusudiwa kuoana. Lakini kama Sulema anavyosema katika Mithali 16, kuna mfululizo katika kutumaini na kujibidisha kunakomheshimu Bwana na kutupa pumziko la kweli. Ni kifungu hicho ambacho tutakiendea katika siku tatu zijazo.


Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Trust, Hustle, And Rest

Biblia inatuagiza kufanya kazi kwa bidii, lakini pia inatuambia ni Mungu-- siyo sisi --anayetoa matunda ya kazi yetu. Kama mpango huu wa siku nne utakavyoonesha, taaluma ya kikristo lazima ikubali mvutano kati ya “kuamin...

More

Tungependa kumshukuru Jordan Raynor kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.jordanraynor.com/trust/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha