Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 02/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

SIKU 1 YA 29

Lengo la Mungu kuwakomboa Waisraeli kutoka utumwani Misri lilikuwa ni kuwarudisha kwake. Kwao ni kule ambako Mungu alikusudia waweko tangu asili. Mungu anataka warudi huko. Anawakumbusha asili yao ni kwa Mungu:Mmeona ... jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi(m.4). Pale alipo Mungu, ndipo anapenda na watu wake wawepo. Upekee wa taifa la Mungu unaonekana pale tu, wanaposikiliza maagizo ya Mungu na kuyafuata. Taifa la Israeli ni kielelezo kwa mataifa yote duniani. Uteule huu unaambatana na kuwajibika na kuishi kwa kufuata utakatifu wa Mungu. Zingatia zaidi jambo hili, ukitafakari ilivyoandikwa katika 1 Pet 2:5 na 9:Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. …Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu c...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha