Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mwongozo wa KiMunguMfano

Divine Direction

SIKU 5 YA 7

Tumika

Kutumikia wengine haiji hivihivi kwangu. Ni mtu nayejifikiria mwenyewe. Ninapenda nilivyo. Si kitu nachojivunia, lakini bahati mbaya, ni kweli.


Mimi siko peke yangu. Sisi wote tunaweza kuwa watu wa kujifikiria wenyewe. Kwa asili sisi ni watu wabinafsi. Hebu fikiria, mtoto huhitaji kumfundisha kuwa mbinafsi. Kulingana na Yesu, maisha si yote kuhusu sisi, na bado kila kitu katika asili yetu( ikiwa ni pamoja na sehemu za chakula) zinatuambia tufanye kwa nia zetu.


Moja ya njia za haraka za kumsahau Mungu ni kuliwa na "nafsi." Yesu aliwaambia waziwazi wale wote waliotaka kumfuata. Alisema, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate." Mathayo 16:24


Mungu anataka tupate Njia yake. Na hazungumzi habari ya nyama zaidi, shika hata mchicha.


Kwa habari ya chakula, Yesu alitoa tamko ambalo litatufanya kusita kabla hatujaagiza chakula. "Chakula changu ... ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake."Yohana 4:34


Hebu fikiria kuweza kusema, " Chakula changu ni kumtumikia Mungu. Chakula changu ni kumpendeza yeye. Chakula changu ni kutimiza kazi Mungu aliyonituma kuifanya. Chakula changu ni kufanya mapenzi ya baba yangu na kumaliza kazi yake." Hiyo ndiyo lishe. Huko ni kuishi kwa mwelekeo wa kiungu.


Wakati desturi zote zinasema, "Jishibishe," Mungu anakwambia washibishe wengine.


Wakati watu wanaotuzunguka wanasema, Kusanya vyote unavyoweza! Jiangalie mwenyewe," Mungu anatutaka tutoe badala ya kula. Wakati desturi zote zinasema, " Shiba mwenyewe", Mungu anataka tuwashibishe wengine. Mungu hakutuumba kuwa wachukuaji. Alituumba tuwe watoaji. Kuliko kuangalia mahitaji yetu wenyewe, tumeitwa kuangalia mahitaji ya wengine. Badala ya kukatisha mstari na kwenda mbele ya wengine, tumeitwa kusubiri mpaka mwisho. Mungu alituumba kutumikia.


Miasha ya namna hii yatabadirisha hadithi yako.


Hebu fikiria. Habari ambazo unapenda kuzikumbuka ni zile za wakati ulipomsaidia jirani, ulitumika kanisani, au ulitoa kitu. Ni kwa sababu tuliumbwa kutumika kama Yesu alivyofanya duniani. Uamuzi wa kutumika unaweza usionekane ni wa asili kwako. Haikuwa hivyo kwangu. Lakini nimetambua kwamba kutumika siyo kitu tunafanya. Mtumishi ndivyo tulivyoitwa kuwa. Kwa sababu tunapotumika, tunafanana na Kristo.


Omba: Mungu, unaniitaje kutumika? Unaniita nimtumikie nani? Unaniita nitumike wapi?


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Divine Direction

Kila siku tunafanya maamuzi ambayo yana unda hadithi ya maisha yetu. Maisha yako yangekuwaje kama ungekuwa bingwa wa kufanya maamuzi? Kwenye Mpango wa Biblia wa Mwongozo wa kimungu, mwandishi mzuri wa New York Times na M...

More

Kungependa kumshukuru mchungaji Craig Groeschel na LifeChurch.tv kwa kuweshesha mpango huu Kwa maelezo zaidi tafadhali temembelea: http://craiggroeschel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha