Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Msalaba Na PasakaMfano

Msalaba Na Pasaka

SIKU 3 YA 7

Kuwekwa Huru kwa Uhuru

Mojawapo ya kazi ambazo nilipaswa kufanya katika seminari ilihusisha kuandika insha iliyopanuliwa ambayo inatoa tafsiri yako mwenyewe au tathmini au hoja ya utafiti. Ninakumbuka insha hii kwa sababu nilijivunia kazi yangu nilipo iwasilisha. Nilikuwa nimedhibiti vifaa vyote vya kuandikia, nikachambua vipengele vyote vya kipekee ambavyo vingeweza kuwepo vinavyoweza kuleta mageuzi katika hoja.

Hata hivyo, niliporudishiwa insha yangu kutoka kwa profesa wangu, kulikuwa na sufuri kubwa, nene, nyekundu juu, pamoja na muhtasari mdogo chini, “Tony, kazi nzuri. Maandalizi makubwa. Mgawo usio sahihi."

Haikuwa kwamba sikuwa nimefanya kazi nzuri; ni kwamba nilikuwa nimefanya kazi ambayo isiyo sahihi. Kwa sababu hiyo, sikupata alama kwa nilichokuwa nimefanya. Ukristo sio tofauti. Sio kwamba hakuna watu wengi wanaofanya mambo mengi bora kama vile, kuhudhuria kanisani, kusaidia wanaoumia, au kusema maneno yote sahihi ya kiroho. Ni kwamba tu wamekosa msalaba. Wamemkosa Yesu Kristo – na wanashangaa kwa nini hawapati ushindi wowote, nguvu, tumaini na mamlaka.

Hii ni kwa sababu sheria za dini zinaweza kuingia katika njia ya uhusiano. Sheria hizi za kidini zinaitwa "uhalali." Inapima hali yako ya kiroho kwa shughuli zako. Lazima kila wakati ufanye zaidi, uwe bora zaidi, uombe kwa muda mrefu na ufanye bidii zaidi. Orodha ya uhalali haina mwisho kwa sababu daima kuna kitu kingine cha kuongeza.

Paulo aliandika maneno makali kwa wale waliokuwa wakitafakari kufuata dini ya Wayahudi katika Wagalatia sura ya tano aliposema,

“Ilikuwa kwa uhuru kwamba Kristo alituweka huru ….”

Sala: Bwana, ninachagua kuishi katika mwanga wa uhuru ambao Kristo alikufa ili niupate. Asante kwa kuniweka huru kutoka kwa kanuni za dini ili niweze kukutumikia kwa moyo wa shukrani. Katika jina la Kristo, amina.

Mtafute Yeye, Uwatumikie Wengine

Wakati ambapo utakuwa kwenye mazungumzo na mtu ambaye anaonekana kung’ang’ana na orodha ya sheria zilizotungwa na mwanadamu, tumia fursa hiyo kushiriki nao ukweli wa ukombozi wa Kristo. Tazama leo njia unayoweza kumhudumia mtu nyumbani kwako au kazini kupitia zawadi maalum. Tumia uhuru wako kuathiri mtu mwingine kwa wema kutoka kwa upendo safi kwa Mungu na sio wajibu.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Msalaba Na Pasaka

Tunavaa misalaba shingoni mwetu, lakini tunapaswa kuitumiaje kwa maisha yetu? Kazi ya Yesu ina nguvu ya ajabu kwetu. Bila Ijumaa, hakungekuwa na Jumapili. Pasaka isingetokea bila msalaba. Gundua jinsi msalaba unavyoungan...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha