Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kumwakisi YesuMfano

Kumwakisi Yesu

SIKU 2 YA 3

Katika mchezo wa mpira wa miguu, wachezaji huwa warefu kuwazidi waamuzi. Wachezaji ni wakubwa, wenye nguvu, na wenye uwezo zaidi kuliko waamuzi walio wazee, wadogo, na mara nyingi wasio na umbo la kupendeza. Katika mchezo, wachezaji wanaweza kutumia nguvu zao kukuangusha ... lakini waamuzi wanaweza kutumia mamlaka yao kukuondoa nje ya mchezo.

Usichanganyikiwe kamwe kuhusu nguvu na mamlaka.

Shetani anaweza kukuangusha. Ana nguvu zaidi yako. Lakini hana mamlaka kabisa juu yako ikiwa wewe ni muumini. Bila shaka Shetani anajua hilo, lakini hataki wewe ujue hilo. Kwa hivyo Shetani hujaribu kukutisha kwa uwongo na shinikizo, na kukudanganya ili uamini kwamba ana mamlaka juu yako.

Msalabani, Yesu Kristo alizima, akavunjilia mbali, na kumnyang’anya shetani silaha zake juu ya dhambi na kifo (Kol. 2:13 – 15). Mungu alimkabidhi Mwanawe mamlaka juu ya yote kabisa. Ameweka vitu vyote chini ya Yesu.

Sababu mojawapo ambayo mara nyingi yafanya hatuishi kulingana na ukweli huu ni kwa kuwa tunachanganya maneno “nguvu” na “mamlaka.” Shetani bado ana nguvu. Bado anatawala ulimwengu tunamoishi na ni mshawishi katika maisha ya watu wengi kwa njia nyingi zisizo hesabika. Mbinu zake ni halisi na za uharibifu. Lakini kile ambacho hana ni mamlaka ya kumalizia. Yesu ndiye anayo mamlaka. Yesu ameinuliwa “…juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki..;”

Shetani hana mamlaka wala uwezo juu ya yule ambaye amefungamanishwa naye na yuko chini ya kifuniko cha Kristo aliyefufuka na kuinuliwa. Hii ndiyo sababu Shetani atajaribu kwa muda mrefu na kwa bidii kumzuia yule ambaye ana uhusiano wa kudumu na Yesu. Anajua kwamba iwapo anaweza kukufanya upuuze mamlaka na utawala wa Kristo katika shughuli zako za kila siku na maamuzi, anaweza kukuhadaa, kukudanganya na kukudhuru apendavyo. Hata hivyo, kukiri na kubaki chini ya ubwana na mamlaka ya Kristo kutakulinda kutokana na mashambulizi ya Shetani.

Mungu “alitufanya hai pamoja na Masihi, ingawa tulikuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu. Kwa neema umeokolewa! Tena alitufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye mbinguni, katika Kristo Yesu” (Efe. 2:5 – 6).

Kristo alipokufa, ulikufa pamoja naye. Kristo alipofufuka, ulifufuka pamoja naye. Kristo alipoketi mkono wa kuume wa Baba, uliketi pamoja Naye. Kwa maneno mengine, uliumbwa ufanye kazi katika umoja na utulivu pamoja na Kristo. Ili uweze kupata mamlaka ambayo huja kupitia muungano mkamilifu wa Yesu Kristo—kuleta mbingu kuzaa duniani—lazima ukae ndani yake. Kukaa kunamaanisha kuishi, kusawazisha mawazo yako, chaguo zako na mtazamo wako chini ya mawazo yake Mungu. Inamaanisha kuungana naye na kumheshimu katika kila jambo unalofanya. Mungu hataki watoto wake kufanya ziara za wikendi; Anataka kuwa awe nao daima.

Hii ni sehemu yenye muhimu sana ya maisha ya ushindi ya Kikristo. Unaweza kwenda kwenye ibada zote za kanisa unazotaka, usome vitabu vyote vya kiroho unavyotaka, hata kufanya masomo yote ya Biblia unayotaka. Lakini kuwa na uzoefu wa yote ambayo Mungu amekupangia huja tu kwa njia ya kujifungamanisha wewe mwenyewe chini ya uhusiano wako na kukaa na huyo anaye tawala juu ya yote, huyo Bwana Yesu Kristo ambaye ameiunuliwa juu sana.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Kumwakisi Yesu

Maisha ya Yesu hapa duniani iliisha na upeo mkubwa: Ufufuo wake, kuonekana baada ya ufufuo, na kupaa mbinguni kimwili. Lakini umewahi kujiuliza nini kilitokea baadaye? Yesu anafanya nini siku hizi? Katika kitabu hiki cha...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha