Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 7 YA 7

Niweke huru Kutokana na Wasiwasi

Sala:

Baba Mpendwa, nipe utulivu wa kukubali mambo ambayo siwezi kubadilisha, kubadilisha mambo ninayoweza na hekima ya kujua utofauti. Nisaidie niishi katika wakati uliopo badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu wakati ujao. Wakati akili yangu inapoanza kutangatanga kwa mambo ambayo haipaswi kufanya, fanya jambo la kunirejesha kwa wakati uliopo - iwe kelele kubwa, king'ora, au mtu anayezungumza nami – chochote cha kunirudisha mahali nilipo sasa, Bwana. Nikomboe kutoka kwa mzigo wa wasiwasi na uniongeze imani yangu kwako.

Maombi Yangu - Mahitaji / Maombi

Maombi Yangu Mwenyewe

Hatua za vitendo

1.Fikiria kuhusu tatizo ambalo rafiki au mtu wa familia yako anahangaikia. Andika kile wanachofikiria juu yake na jinsi inavyoadhiri matendo yao na uwezekano wa matokeo ya hatua watakayochukua kwenye safu moja, na matokeo yanayowezekana. Kisha katika safu nyingine, andika mawazo yako, matendo na matokeo kwa tatizo lilo hilo. Angalia jinsi mawazo yanaweza kuathiri matokeo. Sasa tumia utaratibu huu kwa kitu ambacho una wasiwasi kukihusu. Andika wasiwasi wako, mawazo, matendo na matokeo yanayoweza kutokea. Na kisha kile unachoamini kumhusu mtu mwingine ambaye hana shida katika maeneo haya, kile angefikiria, kusema, kufanya na kuwa na uzoefu.

2.Jizoeshe kupumua kwa utulivu. Kupumua kuna nguvu zaidi kuliko vile wengi wetu tunavyofikiria. Wanawake wamepitia leba bila dawa kwa kufahamu na kutumia sanaa ya kuzingatia na kupumua. Unapopumua kwa kina, inaweza kupunguza shinikizo la damu, kusawazisha viwango vyako vya uasidina pia kupunguza kiwango cha cortisol – homoni inayo inayozunguka mwilini mwako. Hii ndio sababu mara nyingi utamsikia mtu akisema, “Vuta pumzi mara kumi kwa kina” kwa mtu ambaye anafadhaika. Au labda umesema mwenyewe. Ikiwa utatenga muda wa kufanya mazoezi ya kupumua kwa kina mara kwa mara, utakuwa na mwelekeo zaidi wa kutumia njia hii ili kushinda wasiwasi wakati wasiwasi inaposhambulia.

Yachunguze mawazo yako yanapoingia. Ikiwa wazo si wazo lenye kuzalisha yaliyo bora au linalokubalika basi liandike chini na libandike kwenye kisanduku chako cha wasiwasi ulichofanya mwanzoni mwa juma. Mwombe Bwana alishugulikie jambo hili na akupe mtazamo wake kuhusu jambo hilo.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

Andiko

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha