Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuomboleza VyemaMfano

Kuomboleza Vyema

SIKU 1 YA 6

Kumpoteza mpendwa kunaweza kutulemaza kihisia na kutoa changamoto kwa imani yetu hata na mtazamo wetu wa ulimwengu. Wengine wameniuliza kwa miaka mingi ni jinsi gani nimeendelea mbele licha ya kuwapoteza baadhi ya watu tofauti wa familia yangu. Wanapo niangalia kwa umakini ninapoomboleza, huona kwamba sijavurugika. Ingawa baadhi ya hayo yanaweza kuwa yamefungwa katika utu au jinsi ninavyoshughulikia mambo, naamini kwamba sababu kubwa zaidi ni hii, naamini ninachohubiri. Ninaposema “Mungu amedhiti hili,” ni kwa sababu yeye hufanya hivyo kihakika. Ninapokumbuka wale walionitangulia, mimi hufarijika kujua jinsi maisha yamekuwa bora kwao na jinsi yatakavyokuwa bora kwangu wakati wangu utakapofika.

Ningekuhimiza, kama mshipi, ujifunge mwenyewe katika kile unachoamini. Tafakari kuhusu ahadi ya Mungu ya maisha bora baada ya kifo. Mruhusu awe nanga yako, ambapo hakuna kitu kinachoweza kukutikisa, hata si huzuni. Kwanza, Mungu ni mkuu, ambayo ina maana kwamba yeye anadhibiti kikamilifu kila hali. Pili, Ana siku za usoni zilizojaa utukufu wakati zinazowangojea wale ambao wameweka tumaini lao katika Mwana wake, Yesu Kristo. Ikiwa kwa kweli unaamini hivyo, haipaswi kuwapo na kitu chochote ambacho dunia hii inaweza kutupia ambacho kinaweza kukufanya usambaratike.

SALA: Baba, tujaze na ufahamu wa kina zaidi kuhusu nafsi yako. Imarisha imani yangu kwako. Niruhusu nione kwamba wakati kifo kinapomchukua mtu ninayempenda, mkono wako haujawahi ondoka kwenye hali hiyo. Una mpango kwa ajili yetu sisi sote tunaokuamini, mpango unaohusisha kuwepo kwa utukufu mkamilifu milele katika uwepo wako wa upendo. Lisha nafsi yangu huku nikiomboleza kufiwa na mtu ninayempenda. Katika jina la Kristo, amina.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kuomboleza Vyema

Huzuni huja kama sehemu ya asili ya maisha. Unapompoteza mtu unayempenda, inaweza kuwa vigumu kujiongoza katika mchakato wa kuomboleza. Kupitia mpango huu wa kusoma, Tony Evans anazungumza kutoka moyoni mwake kulingana n...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha