Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kumchukua Mungu Kwa UzitoMfano

Kumchukua Mungu Kwa Uzito

SIKU 1 YA 3

Je, inamaanisha nini kuwa na agano na Mungu?

Agano ni uhusiano unaofungamana katika hali ya kiroho ulioamriwa na Mungu ambao kupitia huo anaendeleza ufalme wake. Ni utaratibu ambao kwa huo, yeye hutumia kutimiza makusudi yake, malengo na ajenda zake. Ni mpangilio wa uhusiano, sio tu mkataba rasmi. Unapounganishwa na Mungu katika agano lake, unapata kujua siri zake. Anakuruhusu uingie kwenye mambo ambayo wengine hawajui.

Ikiwa umefunga ndoa, unajua jinsi ilivyo kuwa na siri ambazo unashiriki na mwenzi wako pekee. Kama wanandoa, mnashirikishana matumaini na mawazo yenu ya ndani. Haya ni mambo yaliyofichika na yanayofikiwa kwa asili ya uhusiano wa kiagano wa ndoa. Kwa kweli, siri hizi mara nyingi huthaminiwa sana na kulindwa hivi kwamba mara nyingi husemwa kwa minong'ono. Unahitaji kuwa karibu, si tu kimahusiano bali mara nyingi kimwili, ili kushiriki siri.

Tunaweza kumkaribia Mungu kwa kumcha (Mithali 9:10). Unapofanya hivyo, anakuruhusu uingie na kujua siri zake. Uhusiano wa agano hukuleta karibu vya kutosha kusikia kunong'ona kwake anapofichua makusudi na ahadi zake kwa maisha yako unapokuwa karibu naye.

Kuna tofauti gani kati ya kumcha Mungu na kumwogopa Mungu?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kumchukua Mungu Kwa Uzito

Kwa sababu tumepata upendo na neema nyingi za Mungu, ni rahisi kuwa mlegevu kuhusu utii. Hatumchukulii Mungu kwa uzito vya kutosha. Tunaacha kumcha na hatuzingatii matokeo ya kutotii kwetu. Mruhusu mwandishi Tony Evans a...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha