Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo MajonziMfano

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

SIKU 7 YA 7

Chukua Upanga wa Roho

Hebu tuombe;

Bwana, huzuni inayohusiana na hasara hii ni ya kuponda. Ninajua nitapitia hili, lakini hadi nifanye hivyo, ninakutegemea wewe sana. Ninachukua upanga wa Roho—Neno Lako—na kupata faraja katika huzuni yangu. Ninatumia upanga huu kubatili kila jaribio ya adui kupata nafasi katika maisha yangu. Najua maumivu haya hayatadumu milele kwa sababu nimechagua kuweka tumaini langu kwa wema wako na uwepo wako. Neno lako linasema, "BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa." Zaburi 34:18. Neno lako pia linaniambia kuwa nimebarikiwa katika hasara na huzuni kwa sababu nitapata faraja. Mathayo 5:4. Ninainua kweli hizi ili huzuni na hasara ambayo Shetani anatafuta kuzidisha maishani mwangu itanifanya tu kubarikiwa zaidi na kuwa karibu zaidi na Mungu. Asante, Mungu, kwa upanga wako wa kweli. Katika jina la Kristo, amina.

Zana ya Utumiaji

Omba na umwulize Mungu akufichulie mawazo yako yoyote, imani, au maneno ambayo yanaonyesha roho ya kukata tamaa na kujiuzulu katika kukabili huzuni au hasara. Fikiria mambo ambayo unaweza kuwa umeyasema au kufanya yasiyo akisi imani katika mkono mkuu wa Mungu katikati ya maumivu haya. Andika haya yote.

Kwa kila uwongo, tafuta ukweli unaoupinga kutoka kwenye Neno la Mungu. Unapoandika ukweli unaopingana na ule uongo, hakikisha umefuta uwongo huo na kufanya sala, katika jina la Kristo, kwamba haitaathiri maisha yako na maisha ya wale wanaokuzunguka. Kisha mshukuru Mungu kwamba nguvu ya kweli yake imeachiliwa huru kufanya kazi yake ya uponyaji, kutia nguvu na neema ndani yako. Hapa kuna mfano.

Uongo: Sitaweza kamwe kuachilia na kuondokana na hili.

Ukweli: “Huwaponya waliovunjika moyo, na kuzifunga jeraha zao” (Zaburi 147:3).

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Siku Saba Za Kufanya Sala Wakati Upitiapo Majonzi

Siku 7 za Sala zimeundwa kwa minajili ya kuimarisha roho yako na kuhimiza moyo wako wakati upitiapo majonzi. Kila siku inajumuisha sala utakayofanya wewe au kutumia kama msingi wa maombi yako kuhusu mada ya siku hiyo ili...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha