Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Fukuza HofuMfano

Fukuza Hofu

SIKU 1 YA 3

Je, una utayari wa kujifunza jinsi ya kubomoa ngome ya hofu ambayo adui amejenga ndani ya moyo na akili yako? Yesu alikupa jibu. Unaibomoa kwa kubadilisha vile unavyo vipa umuhimu kwanza. Hiki ndicho hasa alichokuwa anazungumzia katika Mathayo 6:33 aliposema, “Utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Kwa maneno mengine, ikiwa utatumia muda na nguvu zako kujipatanisha na kile ambacho Mungu anafanya katika kuendeleza ufalme wake duniani, anaahidi kuyashughulikia mambo mengine maishani yanayokuhusu ambayo yanaweza kukufanya uwe na hofu au wasiwasi. Yesu alisisitiza hili aliposema, “Msisumbukie ya kesho; kwa maana kesho itajijali yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha” (Aya 34).

Mungu anakupa neema siku moja baada ya nyingine. Neema ya kesho, hatakupa leo, na wewe huna haja nayo. Kwa nini? Kwa sababu Neno lake linatuambia, “Rehema zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi; uaminifu wako ni mkuu” (Maombolezo 3:22–23). Kwa hivyo ikiwa una hofu na wasiwasi kuhusu kile kitakachotokea kesho, kimsingi unamwambia Mungu kwamba haumwamini. Unamwambia kwamba yeye si wa kuaminika. Na kwa kufanya hivi, unatuma mawazo yako mwenyewe katika mzunguko wa maumivu na hofu ambayo itaongeza tabia yako ya mazoea badala ya kukusaidia kushinda. Kuhofia kesho ni kupoteza amani na ushindi wako leo. Acha iende.

Bwana mwenye neema, nisaidie kutambua wakati hofu inanyemelea na kuingia katika mawazo yangu. Nisaidie kuyateka mawazo haya kabla hayajaongezeka na kuwa mengi. Nipe hekima ya kupambanua kilicho busra na kisicho cha busara. Na katika mambo yote nipe uwezo wa kuamini kuwa wewe unanilinda na kusimama nami. Nataka nikutwike hofu zangu kwako, kwa hivyo tafadhali nipe neema ya kufanya hivyo leo na kila siku. Katika jina la Kristo. Amina.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Fukuza Hofu

Unaweza kushinda hisia za hofu. Dkt. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu wa usomaji wa kupata ufahamu. Gundua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukitaka, unapotumia kanuni zilizowekwa kati...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha