Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

SIKU 1 YA 6

Mshipi wa Ukweli

Hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Marko 10:8

“Moja ya vipengele vya utawala wa Mungu ni moyo wake kwa ajili ya umoja, unaojulikana pia kama ulinganifu. Ulinganifu unaweza kufafanuliwa kwa maneno rahisi kama umoja wa kusudi. Ni kufanya kazi pamoja kwa mapatano kuelekea maono na lengo la pamoja.” Tony Evans

Bwana mpendwa, umoja katika ndoa yetu ni zaidi ya kukubaliana tu kuhusu mambo. Neno lako linatuambia kwamba umoja wetu unakuakisi wewe kwa wengine. Kwetu sisi kutokuwa na umojakwaonyesha jinsi tulivyo mbali nawe katika maisha ya kiroho na tabia zetu. Utusaidie tuwe na mawazo ya umoja ambayo yamefungamanishwa na kweli ya Neno lako, badala ya kuona maamuzi yetu na kutoelewana kuwa ni ushindani wa mawazo na hiari.

Yesu alieleza kusudi la umoja aliposema, “Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; (Yohana 17:23). Umoja ni njia yetu ya kushiriki na kuthibitisha upendo wako sio tu kwa Kristo na kwamba ulimtuma, bali pia kwa sisi sote.

Yesu alisema ‘tumekamilishwa katika umoja”. Kwa kuwa iko hivyo, sisi tu mbali na kukamilishwa tunapogombana au kushikilia sana matamanio au maamuzi yetu, bila kujali mwenzi wetu. Nisaidie—tusaidie— tukamilishwe kiroho kwa mchakato wa utakaso wa umoja katika ndoa yetu. Katika jina la Kristo, amina.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Maombi Kwa Ajili Ya Umoja Katika Ndoa Yako

Moja ya matamanio makubwa ya wanandoa ni umoja. Kwa kushangaza, hii imeonekana kuwa ya kuteleza sana. Mara nyingi, tofauti za maoni zinapoingia, matokeo yake ni migogoro, kukata tamaa na kuumia. Katika hali kama hizi, we...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha