Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Gundua Kusudi LakoMfano

Gundua Kusudi Lako

SIKU 1 YA 5

Je, umewahi kwenda kwenye friji yako kutafuta kijiti cha siagi ule? Ulihisi njaa ikigunaguna ndani ya tumbo lako na kwa hivyo ukafikiri, "Kama ningeweza tu kupata kipande cha siagi ningekuwa sawa."

Pengine si hivyo. Hii ni kwa sababu siagi yenyewe haina ladha nzuri sana. Kwa kweli unga, chumvi, soda ya kuoka au viungo vingi vya kupikia havina. Lakini mjuzi anapozikusanya zote pamoja na kuzichanganya, huzichanganya kuelekea kusudi lililokusudiwa. Baada ya hapo, huziweka kwenye joto la oveni na harufu ya keki iliyookwa hivi punde huwavuta wote jikoni.

Andiko linalonukuliwa mara nyingi ni Warumi 8:28 ambapo tunasoma, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

Hata hivyo, sehemu ya kifungu hicho ambayo hunukuliwa kwa urahisi mara nyingi ni, “Mambo yote hufanya kazi pamoja kwa wema.” Tatizo ni kwamba mambo yote hayafanyi kazi pamoja kwa wema. Kunukuu nusu tu ya aya ni kukosa maana nzima. Mambo yanayofanya kazi pamoja kwa wema ni yale mambo yanayohusiana na wale watu wanaompenda Mungu na walioitwa kulingana na kusudi lake. Mungu ana kusudi na wewe nayo hatua ya kwanza katika kuigundua ni kujisalimisha kwa ukweli huo.

Ni wakati tu unapoishi kulingana na kusudi lake - badala ya kusudi lako mwenyewe, ndipo Yeye atasababisha vitu vyote katika maisha yako kuunganika kwa manufaa yako na utukufu wake. Vinginevyo, mambo “yote” bado yanaweza kutokea kwako, ila hayataunganishwa kimakusudi na kusababishwa kufanya kazi kuleta wema wake kwako.

Leo, ikiwa unahisi kuwa maisha yako ni kama aina ya siagi, au maisha yako ni kama aina ya unga, au hata aina chumvi - hatua ya kwanza ya kuelekea kugeuza hicho kuwa kitu kitamu ni kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu na kutafuta kusudi lake kwa ajili yako. Unapokuwa umejitoa kwake, zaidi ya yote, atachanganya mambo yote katika maisha yako - mazuri, mabaya na machungu - na kugeuza kuwa kitu cha kimungu.

Sala:

Bwana, fungua macho yangu nione kusudi lako katika maisha yangu. Nisaidie kusalimisha kwako chochote ambacho sijafanya hivyo na unifichulie wema unaotokana kwako wewe unapounganisha matukio katika maisha yangu ili kunileta kwenye hatima yangu.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Gundua Kusudi Lako

Katika mpango huu wa kusoma kwa ufahamu, mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anakupitisha katika mchakato wa kugundua kusudi lako.

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha