Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya MihemkoMfano

Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya Mihemko

SIKU 1 YA 3

Jinsi Mihemko ilivyo katika nafsi, ndivyo hisia zilivyo katika mwili. Mihemko hufunua jinsi tunavyohisi kuhusu hali za maisha. Watu ambao wamekwenda njia isiyofaa kwa habari ya mihemko yao, hujitahidi kuishi na huenda wakahisi kutokuwa na msaada, wasio na tumaini, na thamani.

Ngome ya kihisia haimaanishi kuwa na siku mbaya kila baada ya muda fulani. Ina maana ya wakati ambapo huwezi kutikisa mtego mbaya ulionasa maisha yako, na kusababisha uvunjike moyo usikoweza kuudhibiti, kufinyilika na huzuni.

Badala ya kufanya kile watu wengi hujaribu kufanya, (ambayo ni kujaribu kukana, au kukandamiza ngome hizo za mihemko hiyo, kwa madawa ya kulevya, burudani, ngono, au kujinunulia watamanicho), nataka nikusaidie ugundue mzizi wa hayo unayopitia ili uyashinde. Ukweli ni kwamba Mungu hakukuumba ili ubebe ngome za mihemko kwa miaka mitano, ishirini, au arobaini au kwa wakati wo wote ule.

Badala yake, Mungu amekuahidi, katika Kristo, uzima tele. Yesu alisema, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” (Yohana 10:10b). Hakukuita ili uishi kila siku ukiwa umeshindwa. Anataka ujue na kuamini kwamba Yeye ndiye anatawala vitu vyote, na kwamba anayachunga maisha yako. Ikiwa haufurahii uzima tele ambao Kristo amekupa bure, ni wakati wa kugeuka. Mgeukie Mungu, mwombe afichue eneo ambalo Imani yako imekuwa pungufu na kwa njia hiyo ngome ya kimihemko yaweza kuwa imeingia. Anataka kukusaidia ujifunze jinsi ya kuona zaidi ya huzuni yako – na kuona maisha katika upeo wake. Anaweza kufanya muujiza kutokana na kile kinachoonekana kuwa fujo.

Je! Kuna mihemko inayoonekana kuwa imeyanasa maisha yako? Je! una utayari wa kuyakabidhi kwake Mungu?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya Mihemko

Wakati ambapo maisha yako yanatoka katika upatanisho wa neno la Mungu, hakika ni kwamba, utakabiliwa na hali ngumu yenye matokeo yaletayo uchungu. Mihemko yako inapokosa kudhibitiwa nayo ikaanza kuamua ustawi wako, utaji...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha