Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 7 YA 31

Mazao yote yameumbwa na Mungu. Mungu anapenda mazao haya yatumike kwa utukufu wake. Wote wanywao kileo wanaonywa. Pombe huondoa hekima maishani. Hakuna mlevi aliyefanikiwa, kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, na utepetevu humvika mtu nguo mbovu (Mit 23:21). Madhara ya ulevi ni kukosa upendo (ling. na Yesu anavyosema kuhusu mtumishi mbaya katika Mt 24:49, Akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi). Moyo wa mlevi hulemewa, naye hushindwa kuitambua na kuifuata nia ya Mungu. Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na lafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya (Lk 21:34). Ulevi huondoa heshima mbele ya Mungu na jamii. Badala ya kujazwa ulevi wa pombe, watu wa Mungu wajazwe Roho Mtakatifu (Efe 5:18, Msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha